TAARIFA ZA AWALI KUTOKA CHADEMA KUHUSU MBUNGE WAO ANAYEDAIWA KUMAMATWA AKIGAWA HELA HUKO KALENGABy Kurugenzi ya Habari: Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili alikuwa akifanya kikao cha ndani Kijiji cha Kitawaya, Kata ya Luhota, ghafla yeye pamoja name makamanda wengine wanawake aliokuwa nao pamoja wakazingirwa na kikosi cha Green Guard vijana wa CCM.

Wakaanza kumpiga na kumdhalilisha vibaya kisha wakampeleka ofisi za CCM Mkoa wa Iringa kwa maelekezo ya viongozi wao kitaifa na mkoa waliokuwa kwenye mkutano wao was kufunga uliofanyika eneo la Kidamali.

Sasa baadae wakagundua kuwa suala hilo litakuwa gumu kwao ndiyo ikatungwa hiyo propaganda ya kwamba wamemkata kwa rushwa il I wajenge uhalali wa kumpiga na udhalilishaji waliomfanyia.

Polisi walienda kumchukua Mama Kammili akiwa ofisi ya CCM Mkoa ambako walikuwa wakiendelea kumdhalilisha.

Tunafuatilia kwa makini na kina suala hili na tutaendelea kuwapatia taarifa.

CCM iko kwenye wakati mgumu sana wa kukabiliana na ukweli wa kushindwa uchaguzi was Kalenga na kukataliwa na wananchi mchana name usiku.

Ni sawa na mtu anayetapatapa kufa maji.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.