TIGO REACH FOR CHANGE YAWAZAWADIA WATATU DOLA 25000 KILA MMOJA KWA KUENDESHA MIRADI YA KUBORESHA MAISHA YA WATOTO.CHEKI HAPA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga akizungumza wakati wa makabidhiano hso ysliyofsnyiks jijini dar es salam leo


            Tigo leo imechagua na kutangaza washindi watatu watakao pewa dola 25,000 kila mmoja chini ya mradi wa Tigo Reach for Change ulio zinduliwa mwezi Novemba mwaka jana yenye malengo yakuboresha maisha ya watoto nchini.

faraja nyalandu ambaye ni mmoja kati ya washindi hao akipokea mfano wa hundi leo


             Wajasiriliamali jamii hao watatu walioshinda ni:-----


       
          1-----Faraja Nyalandu, namradi wa Shule Direct;
‘Shule Direct’ inamalengo yakuhamasisha na kuhakikisha kwamba mtaala  bora yaelimu inapatikana kidigitali kiurahisi na kwa ufanisi zaidi kupitia njia ya simu za mkononi (SMS na kwa kupiga) kwa ajili ya maendeleo mema ya wanafunzi wakitanzania.

2. 
                 2-------   Joan  Avit na mradi wa Grapho Game Tanzania; ‘GraphoGame’ ni mchezo wa watoto uliowekwa kwenye mfumo wa kompyuta (apps) inayoweza kutumika kwa njia ya simu yenye malengo ya kuwawezesha watoto kujua kusoma na kuandika. Imewekwa kwanjia ya mchezo ili kuweza kuwa fanisi zaidi kwa kuwafurahisha na kuwashirikisha watoto pindi wanapokuwa wanajifunza.

3.  
                  3-----  Carolyne Ekyarisiima na mradi wa Apps and Girls;‘Apps and Girls’ina malengo ya kuwa hamasisha wasichana na wanawake kuweza kuelimika zaidi katika masuala ya Teknohama.

nawashukuru sana tigo na reach fo change


“Kutoa huduma za kijamii ni moja kati yangu zao kuu katika kampuni yetu, na tumejikita sana katika mradi huu ambao ni mpango maalum ndani ya mitandao wetu dunia ni kote. Tigo Tanzania imepokea miradi mizuri mengi sana na tumeweza kufanya mchujo mkali sana. Washindi watatu walioshinda siku yale hawakuwafurahisha tu jopo la majaji walio kamilisha zoezi hili bali majaji walipima nakuona kwamba miradi yao yana mantiki na yenye uwezo kiukweli kukabili matatizo ya watoto. Washindi hawa watakuwa wanapokea dola 25,000 kila mmoja kwa mwaka kwa muda wamiaka mitatu kwa ajili ya kukamilisha malengo ya miradi yao,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga.


      Aliendelea kusema, “Ushirikiano wa Tigo Reach for Change unamalengo ya kutambua na kuwawezesha wajasiriliamali jamii wenye mawazo yakibunifu yenye uwezo wa kuboresha maisha ya watoto nchini Tanzania. Washindi hawa watatu wataingizwa rasmi kwenye mpango maalum wa miaka mitatu ambao utawawezesha wajasiriliamali jamii hao kupata ushauri kutoka kwa wataalam wetu ya namna bora ya kuendesha mradi yao. ”

Carolyne Ekyarisiima ambaye pia ni mshindi


Novemba mwaka jana, Tigo ikishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach for Change ilizindua kwa mara ya pili mradi wenye malengo ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasirialamali jamii ambao wangekuja na miradi mizuri na yakibunifu yenye uwezo wakuboresha maisha ya watoto nchini.

       “Baada ya kukaribisha maombi ya mradi kwa muda wa mwezi mmoja, tulipokea maombi 1,100, ambapo 15 ndio walioweza kutinga fainali baada ya mchujo mkali sana kufanyika na ulioendeshwa na wafanyakazi wa Tigo na Reach for Change, pamoja na msaada wa wataalam kutoka nje.

         Wanafainali hawa waliweza kutetea miradi yao mbele ya jopo la majaji ambao nao walivikwa na jukumu zito la kuchagua washindi watatutu kati ya hao,” alisema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.