Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za 'Tigo Ngorongoro Marathon' zitakazofanyika 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, Ngorongoro - Arusha. Kushoto ni Mratibu wa mbio hizo, Datus Joseph, kutoka kampuni ya utalii ya Zara Tours. |
Mwaka
wa saba wa ‘Tigo Ngorongoro Half Marathon’ iliyopewa kauli mbiu ya “Kimbia
kuikabili Malaria” itafanyika Jumamosi ya 19 Aprili 2014 wilayani Karatu,
jijini Arusha. Mbio hizo za kila mwaka inategemea kuwavutia wanariadha 3000 wa
kitaifa na kimataifa, Tigo ilitangaza leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo
John Wanyancha, alisema kwamba Tigo Ngorongoro Marathon ni fursa ya kuhamasisha
jamii kuhusu jinsi ugonjwa wa Malaria unavyoathiri watu milioni 300 mpaka 500
duniani, asilimia 90 wakiwemo barani Afrika.
“Malaria
inaua zaidi watu milioni moja kila mwaka. Nchini Tanzania mtu mmoja anafariki
kwa ugonjwa wa malaria kila baada ya dakika 10. Mbio za mwaka huu inahusisha
pia harambee yakujenga kituo cha hospitali,” alisema Wanyancha.
Mwaka
wa 7 wa mbio hizi za Tigo Ngorongoro Half Marathon inaambatana na maadhimisho
ya Siku ya Malaria inayoadhimishwa tarehe 25 Aprili kila mwaka. Tukio hilo,
kutokana na maelezo ya Wanyancha inategemewa kuzinduliwa na Waziri wa Maliasili
na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kama mgeni rasmi.
Tigo
inashirikiana na moja ya makampuni ya utalii yanayoongoza nchini kwa jina la
Zara Tanzania Adventures, katika kuandaa mashindano haya, ambapo fedha
zitakazopatikana zitatumika kununua na kugawa neti za mbu, pamoja na kununua
dawa za malaria ambapo zitagawiwa mahospitalini Arusha bure.
Fedha
zitakazochangishwa pia mwaka huu zitatumika kukarabati vituo vya afya vilivyopo
pamoja na kujenga kituo kipya cha afya kitakachoanzishwa Ngorongoro pamoja na
shule ya awali katika vijiji tofauti tofauti kwa gharama ya shilingi milioni
160 jumla, alisema Wanyancha.
“Mbio
za Tigo Ngorongoro half marathon sio tu burudani kwa watu watakaoshuhudia
bali ni sehemu nzuri sana yenye kuhamasisha kuhusu namna ya kujikinga na kutibu
ugonjwa wa malaria kwa jamii inayozunguka maeneo ya Monduli na Arusha kwa
ujumla,” alisema.
Mbio
hizi zinawapa fursa wanariadha kukimbia katika sehemu moja yenye vivutio vya
kipekee duniani, kutoka kivutio cha Ngorongoro mpaka jiji la Karatu. Mbio za
mwaka huu pia inahusisha mashindano ya makampuni ya kilomita 5 kwa makampuni
wenye nia yakuchangia katika harambee hiyo.
Kutokana
na maelezo ya Mratibu wa Mbio hizo, Datus Joseph, kampuni zinazaodhamini mbio
hizi katika ngazi za mashindano ya makampuni ni SBC Tanzania Ltd, CHUCHU, BG
Tanzania, Hans Paul, Mberesero Lodge Tented Camps, Afrika-Safari, Orange gas na
BIL.
No comments:
Post a Comment