.

UCHAGUZI WA KALENGA ULIJAA MATUSI NA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE,LHRC YAMTUHUMU MWIGURU NCHEMBA KWA KUWADHALILISHA WANAWAKE ,SOMA KWA UNDANI HAPA


Martina kabasama ambaye ni mratibu wa SAHRINGON akizungumza na wanahabari mapema leo

         Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC kwa kushirikiana na mtandao wa mtandao wa taasisi zisizo za kiserikali kusini mwa Africa SAHRINGON wamesema kuwa uchaguzi mdogo wa ubunge uliomalizika huko kalenga ulijawa na lugha za matusi,kashfa na udhalilishaji mkubwa kwa wanawake pamoja na vitisho katika kampeni za vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo

          Wakizungumza na wanahabari jijini dar es salaam wakili EMELDA URIO ambaye ni kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC pamoja na MARTINA KABISAMA ambaye ni mratibu taifa wa SAHRINGON wamesema kuwa katika kampeni za uchaguzi huo kituo chao kilishughudia uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama wanawake huku wakisema kuwa viongozi kadhaa walinukuliwa wakitoa matusi kwenye kampeni za uchaguzi huo jambo ambalo wamesema ni kinyume na sheria za uchaguzi wa Tanzania.

          Wamesema kuwa moja ya udhalilishaji mkubwa uliofanywa na viongozi katika kampeni ni naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara MWIGURU NCHEMBA alinukuliwa katika kampeni za CCM mkutano wa tarehe 15 mwezi wa 3 akisema kuwa wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wapo bungeni kwa ajili ya kuwahudumia wabunge wa CHEDEMA wanaume kingono hivyo akawataka wananchi wa kalenga kutokumchagua mgombea wa chadema GRACE TENDEGA kwani naye ataenda kufanya hivyo kama atafanikiwa kuingia bungeni.

         KABISAMA amesema kauli kama hizo ni za kidhalilishaji na za kuwanyongonyesha wanawake kwa ujumla na kukemea kauli kama hizi kwa ni zinaondoa heshima na utu wa wanawake.     
Kaimu mkurugenzi wa LHRC bi EMELDA URIO akizunumza na wanahabari leo kuhusu uchaguzi uliomalizika kalenga
         Aidha kauli za vitisho katika uchaguzi huo zilikuwa kwa kasi sana katikakampeni za vyama vya CCM na CHADEMA huku akitolea mfano mbunge wa arusha mjini GODBLES LEMA ambaye katika kampeni moja alinikuliwa akiwataka vijana kujitokeza kwa wingi siku ya kura ili kulinda kura zao huku akisema kuwa waje na maji pamoja na mambo yao ambayo hakuyaweka wazi ni mambo gani jambo ambalo lilizua hofu kubwa kwa wapiga kura kuwa ni mambo gani mbune huyo anayamaanisha.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.