UFISADI WA MAWAKALA WA BANDARI DAR WAMTOA CHOZI WAZIRI MWAKYEMBE,AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA ASHUGHUDIA UOZO MKUBWA,SOMA HAPA

Waziri mwakyembe akiwasili eneo hilo wakati wa ziara


Na Karoli Vinsent

WAZIRI wa Uchukuzi Dokta Harrisoni Mwakyembe leo amedondosha chozi baada ya kushuhudia hujuma iliyokuwa inafaywa na mawakala wa Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea huduma zao zikisimama na kuwaleta usumbufu watumiaji wa Bandari hiyo.

Hayo yaligundulika leo wakati Waziri wa Uchukuzi Dokta harisoni Mwakyembe alipofanya Ziara ya kustukiza kwenye vituo vya mawakala hao na kushuhudia usumbufu unaotokana na Uzembe kutoka kwa mawakala hao.


“Nimepigiwa simu sana na wananchi juu ya hawa mawakala wa Neah Investiment agency kuwa ni wasumbufu sana,na leo nimekuja kushuhudia huo usumbufu kwahiyo nawaomba muwe watulivu na kunipa ushirikiano”alisema Mwakyembe

Ndipo,Mwakyembe aliingia kwenye Ofisi za Neah Invement agency zilizoko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam na kushuhudia umati wa watu wakiwa  hawajapata huduma yeyote kutoka kwa kampuni hiyo huku wakisema wamefika hapo zaidi ya wiki mbili

“Hafadhari mkombozi wetu mwakyembe umefika uje kushuhudia unyama huu tunaofanyiwa na kampuni hizi maana tumekaa hapa wiki ya pili hiii na hatujapewa huduma yeyote badala yake tunapigwa karenda huku mgari yetu yanakwama tu pasipo sababu”alisema mmoja ya wananchi

Baada ya kusikia kelele hizo kutoka kwa Wananchi ndipo waziri huyo akataka kujua nini tatizo na kuwaita Viongozi wa Kampuni hiyo na kushuhudia Urasimu mkubwa katika kuwahudumia wananchi.

“Nakuomba Meneja utuambie nini Tatizo linalopelekea msongamano wa watu wengi hivi?

Ndipo Meneja  wa kampuni hiyo anayejulikana kwa Jina moja Muhamed  akasema tatizo la msongamano wa watu katika ofisi hiyo ni kutokana na tatizo na mtandao katika kumpyuta.

Ndipo Waziri Mwakyembe akagundua tatizo linalopelekea foleni na adha kwa wananchi ni ukiritimba kutoka kwa mameneja wa Kampuni hiyo kwa kushindwa kuweka benki katika ofisi hiyo iliisiwape tabu katika kulipa fedha kwenda tra.

“Nakupa siku tatu wewe meneja lasivyo nafunga hii ofisi yenu yaani kwaanzia leo alhamini mpaka Jumatatu kama hamtoweka Benki humu ndani basi nitawafungia na msiendelee na Kazi na haya majengo mliotumia pesa nyingi mfugie hata kuku”alisema Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo akashangaa jinsi wafanyakazi wa Kampuni hizo za uwakala kushindwa kufanya kazi kwa kisingizio cha mtandao kuwa na kuwaacha Wananchi wakiteseka

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.