.

KUWA WA KWANZA KUFAHAMU HUDUMA MPYA ILIYOZINDULIWA LEO NA BENKI YAKO YA NMB

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing
  Na Karoli Vinsent
        BENKI  ya NMB katika kuonyesha inawajali wateja wake sasa Imezindua huduma itakayowafanya Wateja wake kufurahia Ubora wa Benki hiyo,Baada ya Kuzindua Huduma mpya ijulikanayo “JIHUDUMIE”
         
        Akizindua Huduma hiyo,leo hii Jijini Dar Es Salaam, mbele ya Waandishi wa Habari na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing alisema Kampeni inayojulikana “Jihudumie ni huduma mpya ambayo itakayowafanya Wateja Wa Benki hiyo kufurahia ubora na Ufanisi.

        
        “Tunakwenda ,kuwambia wateja wetu kwamba wanaweza kutoa fedha muda wowote na mahali popote,NMB inandelea kubuni na kuongeza huduma,kwa kushirikiana na Mitandao ya simu za Mikononi,pamoja Huduma za ATM za Benki hii,zilizotambaa Nchi Nzima”alisema Wiessing
       
            Vilevile mkurugenzi huyo alizidi kusema kwa sasa mteja wa Benki  hiyo ataweza kufungua akaunti ya chap chap chini ya Dakika 10,na kuweza kulipia bili kupitia NMB mobile kama vile Dawasco,DSTV,TRA.
        
         Alifanunua kwa sasa mteja wa Banki NMB,ataweza kutuma kiasi kinachofikia milioni moja kwenda kwenye NMB mobile,ambapo huduma hii ilikuwa tofauti na mwanzo,na vilevile kwa sasa mteja wa Banki ya NMB anaweza kupata Huduma za Kibenki kupitia Internet Banki.   

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.