Meneja
usimamizi wa Barabara toka Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART)
Mhandisi Mohamedi Kaganda (kulia) akielezea kwa waandishi wa
Habar(hawapo p ichani)i leo Jijini Dar Es Salaam namna mabasi hayo
yatakavyofanya safari zake mara awamu ya kwanza ya mradi huo
itakapoanza mapema mwakani , Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari
Maelezo Frank Mvungi.
Meneja
Uhusiano Mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. William Gatambi
(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam
katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu maendeleo ya mradi huo
ambao awamu ya kwanza itakamilika mwishoni wa mwaka huu. Kulia ni Afisa
Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
Meneja
uendeshaji wa DART Bw.Peter Munuo akieleza kwa waandishi wa habari
kuhusu faida za mradi huo ikiwemo kuondoa tatizo la foleni katika jiji
la Dar es salaam na viunga vyake.mara mradi huo utakapoanza mapema
mwakani.
( Picha zote na Georgina Misama )
Na Frank Mvungi- Maelezo
Serikali
inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi
wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni
jijini Dar es salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu kukamilika.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART)
Bw.William Gatambi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam.
Gatambi
alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mradi huo
awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2014 itasadia kufanikisha usafiri
wenye tija kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake.
Miundombinu
hiyo, inajumuisha barabara ya kilomita 20.9 kuanzia Kimara Mwisho hadi
Kivukoni,Barabara ya Kawawa kutoka Morocco hadi Magomeni na Barabara ya
Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo.
Aliongeza
kuwa ina vituo vidogo 27,vituo vikuu vitano, vituo mlisho vine na
karakana mbili. Pia inajumuisha njia za waenda kwa miguu na baiskeli.
Akifafanua
Gatambi alisema mradi wa majaribio utaanza na mabasi 20 yatakayokuwa na
uwezo wa kuchukua abiria kati ya 145 hadi 160 kwa wakati mmoja hali
itakayosaidia kuondoa kabisa kadhia ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar
es salaam.
Aidha,
katika mradi huo wa majaribio Gatambi amesema kutakuwa na mabasi
mengine 10 yenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 50 na 60 ambayo
yatatumika kuchukua abiria kutoka pembezoni mwa jiji la Dar es salaam
kuja katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo Haraka.
Kwa
upande wakeMeneja Usimamizi wa Barabara wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda
amesema mradi huo utasaidia kuondoa tatizo la foleni Jijini Dar es
salaam na kuwafanya wananchi kupata huduma ya usafiri yenye kukidhi
viwango vya Kimataifa.
Pia
Kuganda alisema DART kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Dar es
salaam inafanya maandalizi ya kuboresha barabara mlisho (feeder roads)
katika maeneo yatakayotumiwa na mabasi mlisho.
Katika
mradi wa mabasi yaendayo haraka kutakuwa na Vituo Vikuu (terminals)
vitano 5 katika, maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni
ambapo vituo hivi ndiko mabasi yatakapokuwa yanaanzia na kumalizia
safari kubadilishana abiria kati ya njia kuu na njia mlisho (feeder
roads) ambapo vituo hivyo vikubwa vinatoa nafasi ya kuweza kuanzishwa
kwa huduma muhimu kwenye vituo hivyo kama maeneo ya kukatia tiketi na
vyoo.
No comments:
Post a Comment