HABARI zilizotufikia mda huu,Zinasema
Vurugu kubwa zinatokea kwenye Chuo Cha Kodi kilichopo Mwenge Jijini Dar Es
Salaam,na zimepelekea uharibifu wa Mali.
Kwa Mujibu wa Chanzo chetu cha
Kuaminika kilichopo hapo,kinasema Fujo hizo zimeanzishwa na Viongozi wa
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini wakishinikiza ,Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini(TAHIRISO) bwana Mussa Leonard mdee,
Kujiuzulu kutokana na Vitendo vyake vya kifisadi na Kujiingiza kwenye Masuala
Ya Kisiasa ambapo ni kinyume na Sheria za TAHARISO
Chanzo hicho kilizidi
kufafanua,Mwenyekiti huyo ambae ni Rais Kutoka Chuo Cha Madaktari
Bugando,alitumia pesa vibaya na tena pasipo kuwashirikisha Viongozi
wenzake,na Vilevile kujingiza kwenye Siasa ambapo aligombania kwenye uchaguzi
wa Jimbo la Karenga kupitia Chama cha Demokrasia CHADEMA, na kushindwa kwenye
kura za Maoni.
Ndipo,wajumbe wanaounda TAHIRISO,ambao ni Viongozi kutoka Vyuo Vikuu
mbalimbali hapa nchini walipomuorodheshea makosa hayo, ndipo wakamuengua
Uongozi na kumteua Mwenyekiti mwengine Joseph Moler kutoka Chuo cha Kodi
kushika nafasi hiyo.
Ambapo,baada ya kubadilisha Uongozi
huo,Yule mwenyekiti wa TAHIRISO wa kwanza akagoma kujiuzulu ndipo Wajumbe wakaanzisha fujo na kurushiana viti
ukumbini hapo na Wajumbe wengine wanaomuunga Mkono mwenyekiti huyo .
Chanzo,hicho kiliomba Jeshi la
Polisi kufika eneo hilo.
Habari kamili inakujia
No comments:
Post a Comment