Saturday, May 31, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI---RAIS KIKWETE ATAJWA KUHUJUMU MCHAKATO WA KATIBA MPYA,WANANCHI WASEMA AMEWASALITI.SOMA KIUNDANI HAPA

Wachokoza mada katika mdahalo huo ambao umemalizika muda mchache uliopita,mwanzo ni awadhi ally,Ayubu Rioba,Onesmo olenguruma,na Mwesiga baregu
 Na Karoli Vinsent

        WANANCHI mbalimbali wamtaja Rais Jakaya kikwete kuwa ni kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa Katiba Mpya ,kutokana na kushindwa kusimammia misimamo yake mwanzo ambayo ilikuwa inamalengo ya kupatikana katiba mpya ya Wananchi.

        Hayo,yamegundulika mda huu kwenye Mdahalo wakujadili Katiba mpya,uliondaliwa na Umoja wa Asasi za kirai (AZAKI)uliofanyika jijini Dar es Salaam,mdahalo huo ambao uliwahusisha Wananchi wa Kawaida pamoja na Wasomi Mbalimbali.

       Katika Mdahalo huo wananchi wameonekana Dhahiri kumshutumu Rais jakaya Kikwete kwakushindwa kusimamia misimamo yake ya mwanzo ambayo ilikuwa  inalengo la kupatikana Katiba mpya ya Wananchi  bila Upendeleo,ambapo sasa ameonekana kubadilika na kuanza kushikilia Misimamo yake ya Chama  cha Mapinduzi CCM, ambayo inakuwa kinyume na sasa.
Watanzania waliojitokeza katika mdahalo huo
          Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa Masuala ya kisiasa Nchini kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Profesa Mwisiga Baregu.alisema Rais kikwete amefanya usaliti mkubwa sana kwa wananchi kwa kitendo chake kuanza kufuata maoni ya chama chake.
“Kiukweli mimi sikutegemea Rais kikwete angefanya usaliti namna hii kwenye mchakato huu wakatiba, wakati mimi sikutegemea .Kwanza wakati kila hatua tuliyokuwa tunaifanya kwenye mchakato huu wakatiba tulikuwa tunamjulisha halafu na yeye alikuwa anaungana na sisi kwa kazi tuliokuwa tuanafanya”

       “Lakini tunashangaa yeye amebadilika na kuanza kufuata misimamo ya chama chake,na huku ndiko alipoanza kuharibu mchakato mzima wa ujio wa Katiba mpya.Alisema Baregu.
Baregu,ambaye ni Kada kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,alizidi kusema kitendo cha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.
Kuendelea  kujadili Rasimu ya Muundo wa Serikali mbili ni kuvunja kanuni ya mabadiliko ya katiba kifungu cha 25,ambacho kinataka wajumbe wa Bunge hilo kutojadili Rasimu ya Kwao.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Nchini,Deus Kibamba,aliwataka wananchi kushirikiana na AZAKI ,kutetea katiba yao na kutowaacha wanasiasa kuhodhi mchakato mzima wa Katiba.
Vilevile Mwanasheria na mwenyekiti wa chama cha Wanasheria Zanzibar Hawadhi Ally, ambapo yeye alikuwa miongoni mwa  Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,alisema Rais Jakaya Kikwete ndio mtu wa kulaumiwa kwa wananchi kwa kitendo chake cha kuanza kufuata matakwa ya Chama chake ambao wamekuwa kinara wakubwa wakipinga maoni ya tume ya Jaji warioba.
Mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania Deus Kibamba akitoa maoni yake kama mwananchi katika mdahalo huo uliomalizika muda mfupi uliopita
  
Naye Mwenyekiti wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali,inasimamia Muenendo wa Shuguli za Bunge nchini,Marcus Albanile,aliwataka wananchi kuacha upole wa kuigopo Serikali ya Rais Kikwete,  ambayo imekuwa hikihalibu mchakato wa katiba mpya na akawataka wananchi kuandamana na kulala barabarani na kudai katiba mpya.
Ikumbukwe, Midahalo hii ya kuwapa wananchi fursa ya kujadili katiba mpya imeandaliwa na Umoja Asasi zisizokuwa za Kiserikali AZAKI,ambao umoja huo unawakilisha Asasi hizo zaidi ya mia tano.


No comments: