Wednesday, May 28, 2014

LHRC WAZINDUA KITABU CHA URANI NA MAZINGIRA 2014,MADHARA YA MADINI HAYO YAANISHWA

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania kwa kushirikiana na ROSA LUXEMBURG FOUNDATION  leo wamezindua kitabu cha urani na mazingira 2014.
Akizindua kitabu hiko leo mgeni rasmi bi MOHFAUDHA HAMID ambaye ni makamu mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamuna utawala bora amesema kuwa Tanzania lazima itafakari kwanza maamuzi yake ya kuchimba madini ya urani kwani madini hayo yana madhara kwa binadamu wanaozunguka madini hayo
kitabu hiko kimeainisha mambo yote ambayo ni madhara ya kimazingira na kiuchumi yatokanayo na madini hayo endapo yatachimbwa. 

Bi  HELLEN KIJO BISIMBA ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa LHRC akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho leo jijini Dar es salaam



Mgeni rasmi ambaye ni makamu mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na na utawala bora Hon MAHFOUDHA HAMID akikata utepe kuashiria kizindua Kitabu hiko ambacho kimejaa athari na madhara yatakayoletwa kama tutachimba madini ya urani katika nchi ya Tanzania

No comments: