Sunday, May 25, 2014

MWENGE WA UHURU 2014 WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO, WAMMULIKA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ALIYEKATWA MKONO MWAKA JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati) akishiriki mbio za Mwenge wa
Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa
Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya
kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya
Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe
25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya
maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.
Abass Kandoro Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa leo
tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya
maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne
(4). 
Mkimbiza Mwenge waUhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa
wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa
ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa ng’ombe wawili wa
kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la kulimia wanyama (Plau) jana
tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu
kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa
mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. Kushoto
anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Methew Sedoyyeka.
Ng’ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai waliotolewa msaada kwa Mama Maria Chambanenge.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa
wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa
ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa jembe la kulimia
wanyama (Plau) na ng’ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) jana
tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu
kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa
mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. 
Mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga ambaye alisababishiwa ulemavu
mwingine wa viungo mwaka jana 2013 na watu wasiojulikana baada ya kukatwa mkono
wake wa kushoto kwa imani za kishirikina akishika Mwenge wa Uhuru jana tarehe
24-05-2014 ulipotembelea kijijini kwao kuzindua mradi wa maji na kumkabidhi
msaada wa ng’ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la
kulimia wanyama (Plau) vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa
kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mama huyo. 

No comments: