Kiungo mshambuliaji wa timu ya Al
Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili nchini kujiunga na kikosi cha
Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.
Kazimoto ambaye amewasili nchini
jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo (Mei 6 mwaka huu) kwenda Tukuyu
mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka kambi yake chini ya Kocha Mart Nooij
kujiandaa kwa mechi hiyo.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka huu) ilicheza mechi ya kirafiki na
Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Zimbabwe
(Mighty Warriors). Mechi hiyo dhidi ya Flames ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine na kumalizika kwa suluhu.
No comments:
Post a Comment