Thursday, May 29, 2014

TP MAZEMBE YAWAACHIA SAMATTA NA ULIMWENGU KUJA STARS


SAMATA, ULIMWENGU KUIONGEZEA NGUVU STARS
Klabu ya TP Mazembe imewaruhusu wachezaji wake Mbwana

Samata na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.


Taifa Stars itacheza na Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.

Samata na Ulimwengu watawasili Harare kesho (Mei 30 mwaka huu) saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways. Watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu watakwenda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.


BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: