Thursday, May 8, 2014

WATENGENEZAJI WA BLUE BAND WAANZA KUWAJALI WANAFUNZI NCHINI



Na Karoli Vinsent

        KATIKA kuonyesha inawajali  Wanafunzi wa Shure za Msingi Nchini Kampuni ya Univiler Tanzania Limited,ambao ni watengenezaji na wasambaza ji wa Bidhaa ya BLUE BAND nchini,Imeandaa shindano Bomba likalowafanya Wanafunzi Nchini kufurahia ubora wa Bidhaa hizo.

      Uzinduzi Huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Univiler Tanzania,,mbele ya Waandishi wa Habari ambapo alisema mashindano hayo yatafanyika katika shure zaidi 600 za msingi kote nchini Tanzania.

         “Mashindano haya yatafanyika katika shure za msingi zaidi ya 600 katika maeneo yote ya Tanzania ,na kufikia kiwango cha chini cha watanzania 500,000 na Zaidi ya Walimu 600”

  Wanafunzi wa shule ya Diamond wakiaangalia mfano wa shindano lenyewe

       “Kupitia  promesheni hii,Blue Band itaendelea na Safari yake ya kushirikiana na Kaya na shure ili kuhakikisha kuwa watoto wetu si wanapata zawadi kupitia Bidhaa hii,lakini pia wanapata nafasi ya kujifunza kuhusu  misingi ya Umuhimu wa Lishe Bora kwa kufurahia Kushiriki kwa Vitendo”alisema Banda
         
   Vilevile Banda aliwataka wanafuzni na walimu kujiaanda kupata zawadi nono kutoka kwenye Kampuni hiyo,kwani Zawadi zitaendana na shindano hilo.

        Kwa upande wake mgeni Rasmi ambaye ni Kamishna wa Elimu,kutoka Wizara ya Elimu na Tanzania,DK Leticia Sayi aliwataka wanafunzi na walimu kuchangamkia Fursa hiyo ambayo itawafanya kubadilisha hali za shure pamoja na wanafunzi kupitia shindani hilo.



No comments: