Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Baada
ya watu, wanaojiita Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,kuandamana mpaka kwenda kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali “CAG”
pamoja na kwa Masajili wa vyama vya kisiasa nchini,kuwashtaki viongozi wa Juu
wa chama hicho kwa madai ya matumizi mabaya ya Fedha.
Nae,mwanasheria mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu,ameibuka na kuwataka wanachama wa
chama hicho kuwapuuza watu hao,kwa madai kuwa chadema iliwafukuza uanachama na sasa
hivi wanatumiwa na Viongozi wa kutoka
chama cha Mapinduzi ili kukidhofisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Kauli huyo ya Tundu Lissu,ameitoa muda huu
wakati wa mahojiana na Mwandishi wa Mtandao huu kwa njia ya simu kutoka mjini
Dodoma kwenye Vikao vya Bunge vinavyoendelea huko, ili kutaka kujua kauli ya
chama kuhusu tuhuma hizi,ambapo alisema chama hicho akiamui mambo bila
kuwashirikisha wajumbe wa juu wa chama hicho na pia chadema ilishwafukuza
viongozi hao kutokana na kutumiwa na CCM.
“Kwanza nataka niwambie wanachama wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema ,kwamba madai wanayosema matapeli hao
hayana ukweli wowote na kwanza chama kiliwafukuza uwanachama, mda mrefu,na chama
chetu kinafanya mambo kwa kuzingatia katiba na sheria vilevile kuwashirikisha
wajumbe Kamati kuu ya chama”alisema Lissu.
Kuhusu madai ya matumizi mabaya ya
Fedha ndani ya chama hicho. Tundu lissu alisema anashangaa sana kwa madai hayo
kwani chama hicho kila shilingi 10 inayotumia ndani ya chama hicho,inapitishwa
na kamati kuu ya Chama hicho ,na tena kamati kuu hiyo inakutana kila baada ya
miezi mitatu kukagua.huku kama kukitokea matatizo kwenye matumizi ya Fedha
kamati hiyo inawajibu ya kumwajiisha kiongozi yeyote ambaye atakuwa mesababisha
matumizi.
Lissu,ambaye ni Mbunge
wa Singida Mashariki alizidi kusema endapo chama kingekuwa kinafuja pesa
ingeonekana wazi katika ukaguzi unaofanywa na mkaguzi wa Hesabu za
Serikali,ambapo chama hicho mala zote inapoguliwa haijawai kutokea ufisadi
wowote.
Kuhusu tuhuma wanazodai kwamba Magari
ndani ya Chama hicho yamesajiwaliwa kwa jina Mwenyekiti wa Chama
Freeman Mbowe.
Lissu, ambae ni
wanasiasa mjuzi wa juu wa masuala ya Sheria nchini alisema madai wanayosema
magari yamesajiliwa kwa Jina la MBOWE HOTER sio kweli badala yake chama hicho
kilikuwa kinatumia magari ya Mbowe kabla hajauziwa chadema.
“Ngoja niwaeleze ukweli wanachadema
kuhusu uongo huu unaoenezwa na hawa wasaliti,kwanza hakuna gari lolote
limesajiliwa kwa jina Mbowe,bali yale magari makubwa yaliyokuwa yanatumiwa
kipindi cha kampeni yalikuwa ya Mbowe,tena sisi wenyewe wajumbe wa Mkutano mkuu
kwenye uchaguzi wa mwaka 2005”
“Tulimpigia magoti Mbowe tukampigia
magoti mbowe tukamwomba magari ndio akatupa magari yale makubwa ,akatupa kwa
moyo mmoja na tukayatumia kwenye uchaguzi ule tena baadae sisi wenyewe wajumbe
wa mkutano mkuu akiwemo na huyo msaliti
Yona tuliazimia kuyanunua magari hayo kwa moyo mmoja,nashangaa leo
watu wanavyomtukana mbowe kiasi hichi?alizidi kuhoji Lissu
Kuhusu madeni ambayo
mbowe ameikopesha Chadema ambayo hayaishi.
Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema Tundu
lissu,alisema viongozi hao ni watu wasio kuwa na Fadhila kwa kwenyekiti wa
Chama hicho Freeman Mbowe kutokana na Kazi kubwa aliyoifanya kwenye chama hicho
pamoja na Demokrasi ya Nchini kwa kumchafua Kiasi hicho.
“Jamani hawa watu wananini na Mbowe
kwasababu tangu mwaka 2005 kamati kuu ya chadema ilimwangukia mbowe na kumuomba
hatukopesha Fedha na kweli mbowe alitukoposha milioni 520,kutoka mwaka huo
chama kilimrudishia mbowe milioni 160,tena Mbowe akatusamehe hiyo pesa
iliyobaki sasa hayo madai kwamba mbowe anaiba pesa za Ruzuku kwa kisingizia cha
kulipa Deni alilotukopesha sio kweli”alisema Lissu.
Madai ya Katibu mkuu wa Chadema
Wilbrod Slaa kuchukua Milioni 160 kwa mwaka huku wajumbe wa juu wakichukua sh
0.
Mwanasiasa huyo,
machachari alisema huo ni miongoni mwa uongo ambao chama hicho unafanyiwa kwa
lengo la kuua Demokrasia nchini ambayo ilianza kuonyesha kustwawi miaka ya hivi
karibuni.
“Kwanza ngoje niweke sawa hili kwanza
mnamo Mwaka 2010 sisi wajumbe wa Mkutano mkuu tulimuomba Dokta Slaa agombea Nafasi ya Urais na achane na
nafasi ya ubunge,yeye akasema endapo akikosa nafasi hiyo itakuwaje,sisi wenyewe
wajumbe wa” mkutano mkuu tukamwambia tutakupa pesa ya mshahara wa Ubunge
milioni 7 kwa mwezi,maana yake kwa mwaka anapata milioni 84 sio uongo wa
160,hivi walitaka katibu mkuu hawe masikini?alihoji Lissu
Kuhusu kutofanyika Mkutano mkuu wa
Wajumbe wa Chama hicho
Tundu Lissu,alisema ni
kweli mkutani mkuu haujafanyika kipindi cha mwaka mmoja sasa ambapo ni kinyume
na katiba ya chama.ila sababu ya kutafanya hivyo iko wazi ni kwamba hujafika
mkutano mkuu kwa sababu mwezi wapili huo ungetakiwa ufanyike tulikuwa kwenye
bunge la katiba na akasema kwa sasa chama kiko mbioni kuitisha mkutano huo.
Kauli hii ya Lissu imekuja siku moja
ikiwa Baadhi ya viongozi wakiongozwa Joseph Yonna ambaye anajiita ni
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Temeke na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama
hicho pamoja na Athumani Balozi ambaye naye amejipachika cheo ambacho hakipo
cha ukatibu wa Chadema kutoa mkoani Tabora.
Ambapo waliandamana
Jana mpaka ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali CAG Ludovick
S.L.Utouh,pamoja Msajili wa Vya Kisiasa kwa madai ya Mwenyekiti Freeman Mbowe
Pamoja kutumia pesa vibaya za Chama na kuvunja kanuni za Chama.
No comments:
Post a Comment