Thursday, June 19, 2014

CHINI YA KAPETI: MICHAEL RICHARD WAMBURA RUFAA YAKE YAPIGWA CHINI TFF, AONDOSHWA UCHAGUZI SIMBA SC

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxMoQA6oSCm_esjoyL1qj6cv-KCztc5CQfEhpS7nwMMXQZ8Mhj6BMYEEN_Cb_eSjy5K-cYGPcDTRf6mccJA8JI8alGI7icmLVvltLUJdNxE0Ztm-IWqg5_sDEPMsSV-DMgGjI6VBedclg/s1600/DSC05070.JPG
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

TAARIFA zilizotufikia muda zinaeleza kuwa kikao cha kamati ya Rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, kimemalizika jioni  hii na kuamua kuitupilia mbali rufaa ya Michael Richard Wambura aliyekuwa anapinga kuondoshwa kwa mara ya pili katika uchaguzi wa Simba.
Kwa maana kamati ya Wakili Lugaziya imeungana rasmi na kamati ya uchaguzi ya Simba kuwa Wambura ana makosa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.
Wambura alikuwa mgombea wa nafasi ya Urais ambaye jina lake lilienguliwa na kamati ya uchaguzi kwa mara ya kwanza na alikata rufaa ambapo alishinda na kurejeshwa katika kinyang`anyiro hicho.
Lakini kamati ya uchaguzi ya Simba ilimuengua tena baada ya kubainika amepiga kampeni kabla ya muda.
Wambura alipinga maamuzi hayo na kukata rufani ya pili ambayo imesikilizwa leo na kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF, lakini ameangukia pua baada ya rufani yake kutupiliwa mbali.

No comments: