Monday, June 23, 2014

EXCLUSIVE--CUF WAUNGURUMA DAR LEO,NI KATIKA MKUTANO WAO MKUU,LIPUMBA ASEMA SERIKALI TATU HAZIEPUKIKI,MBOWE NAYE NDANI AKAZIA KUWA UKAWA HAITARUDI BUNGENI--PICHA ZAIDI YA KUMI ZA MKUTANO HUO ZIKO HAPA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM HARUNA LIPUMBA akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho leo muda mchache uliopita wakati akifungua rasmi mkutano wa mwaka wa chama hicho jijini Dar es salaam
 Chama cha wananchi CUF leo kimeanza rasmi mkutanmo mkuu wa chama hicho ambapo pamoja na mambo mengine chama hicho kitafanya uchaguzi wa viongozi wake wa ngazi za juu.

Akizungumza na mamia ya wanachama wa chama hicho mwenyekiti wa CUF IBRAHIM LIPUMBA amesema kuwa chama hicho kijiandae kufanya uchaguzi wa makini ili kupata viongozi ambao watasaidia katika kupata ushindi katika uchaguzi ujao nchini

Akizungumzia swala la katiba na UKAWA kutoka nje amesema kuwa kamwe UKAWA haitakufa,na hawapo tayari kurudi tena bungeni kama wana CCM hawataaxha kujadili rasimu yao na kujadili rasimu ya wananchi kama ilivyopelekwa bungeni,huku akimtaka Rais KIKWETE kuunusuru mchakato huo ulipokwama.

Katika mkutano huo wa mwaka wa CUF umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE na katibu wake DK WILBROD SLAA.

Ishara ya serikali tatu ndio ilmetawala katika mkutano huo ambapo kila kiongozi aliyesimama alikuwa akiwataka wanachama kusema ni serikali tatu pekee 

Makamu mwenyekiti wa CCM BARA PHILIP MANGULA ameiwakilisha CCM katika mkutano huo ambapo katika salamu zake ameonekna kuwapongeza CUF kwa kuwa chama chenye misimamo
SAWA SAWA--katibu mkuu wa CUF akizungumza na wajumbe hao katika mkutano huo
 




FREMAN MBOWE ni mwenyekiti wa chadema na pia makamu mwenyekiti wa UKAWA BUNGENI mbapo alikuwepo katika mkutano huo,amejaribu kuweka wazi misimamo ya UKAWA na kusema kuwa kamwe wana CCM wasidhani kuwa ukawa itarudi nyuma kamwe,muungano huo utaenda hadi katika maswala ya uchaguzi japo hakuweka wazi kama watasimamisha mgombea mmoja japo ameonenekana kuwaomba wana CUF katika mkutano huo wautumie kujadili ni jinsi gani wataimarisha UKAWA ili izidi kuimarika zaidi.

Picha ya pamoja
Katibu mkuu wa CHADEMA akiwa na katibu mkuu wa NCCR mageuzi mosena nyambabe
HABARI ZAIDI KUHUSU MKUTANO HUU ZITAKUWA ZINAKUJIA HAPA HAPA

No comments: