Thursday, June 12, 2014

EXCLUSIVE--KAMISHNA KOVA AELEZEA MOTO WA MCHIKICHINI ULIVYOANZA,SASA WAUNDA KIKOSI MAALUM CHA KUCHUNGUZA

       Jeshi la Polisi Kanda Maalum limeanza uchunguzi cha kuhusu tukio la moto mkubwa uliotokea katika soko la Mchikichini Ilala.

          Tukio hilo lilitokea ghafla majira ya saa tano za usiku ambapo bidhaa mbali mbali za wafanyabiashara ziliteketea kwa moto.  Watu walioshuhudia tukio hilo waligundua motu huo ulianzia katikati ya soko.  Licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na kikosi cha Zimamoto na Shirika la Umeme Tanesco bado moto huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kuteketeza sehemu kubwa ya soko. 

       Jitihada kubwa sana zilifanywa na Kikosi cha Zimamoto na kutoka Jiji, Bandari pamoja na kampuni Binafsi zenye magari ya Zimamoto.  Hali ilikuwa ngumu sana kulingana na bidhaa zilizokuwa zinaungua ikiwa ni pamoja na nguo, viatu, mabegi na vifaa vya plastiki ambao zilichochea moto huo kuenea kwa kasi.

       Kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa ni kuzuia moto huo usisambae katika makazi ya watu jambo ambalo lililokuwa gumu lakini liliwezekana kupitia watendaji hapo juu.

        Jeshi la Polisi lilidhibiti wizi au upotevu wa mali na wahusika walijulishwa wakafika na hata wale wakorofi walidhibitiwa.  Baada ya jitihada kubwa ya ziada moto huo ulizimwa majira ya saa 9.00 usiku huku ulinzi ukiimarishwa hadi asubuhi ya leo.  Aidha hakuna taarifa zozote za watu waliopoteza maisha au kujeruhiwa.

          Mizigo yote iliyookolewa haikuruhusiwa kuondolewa eneo la tukio ili kusubiri uthibitisho wa wanaohusika.  Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha moto huo na kwa kushirikiana na vikosi vyote tajwa hapo juu uchunguzi umeanza mara moja ili kujua chanzo halisi cha moto huo ikiwa ni pamoja na kutumia wataalamu wa kimaabara (Forensic Investigation).


Taarifa kamili itatolewa mara baada ya kukamilika kwa moto huo.

No comments: