Friday, June 13, 2014

HALI NI MBAYA SANA AJIRA KWA VIJANA,CHEKI VIJANA WALIVYOUJAZA UWANJA WA TAIFA WAKITAKA AJIRA ZA UHAMIAJI--HAPA WANAHITAJIKA WATU 70 TUU

               Na Karoli Vinsent

         
  KAULI aliyoisema Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kwamba vijana wasiokuwa na Ajira ni Bomu linalosubiri kulipuka muda wowote,linazidi kujidhihirisha, Baada ya leo Maofisa wa Uhamiaji kuonja  kali ya mwaka, ambayo hawataisahau maishani mwao.

         Hayo yalibuka leo Kwenye Usahili wa Vijana ambao waliomba nafasi ya kujiunga  Jeshi la uhamihaji nchini kwa mwaka huu,ambazo zilifanyika kwenye uwanja  mpira wa Taifa Jijini Dar es Salaam,ambapo vijana hao walikuwa wengi na kujaza uwanja huo kama kuna mechi ya mpira ya Watani wa jadi Simba na Yanga,ambayo imekuwa ikijaza watu kiasi hicho.
 
         Mwandishi wa Mtandao huu, alifika eneo hilo ndipo alishudia kundi la watu likiwa likisubili kufanyiwa usahili,huku vijana hao wakiwa wamechoka kwa kuwangojea maofisa hao ili waje kuwapa mitahani ambayo wanaitumia kwenye usahili.

        Ambapo vijana hao wakitoa malalamiko kwa maofisa hao wa uhamiaji kwa kuwa weka kwa mda mlefu.

      “Kama wanachakachua hayo majina waseme tu,maana tumekaa mda  mrefu sana hapa, akuna chochote kinachofanyika”alisema kijana mmoja ambaye aligoma kutaja jina lake mtandaoni

     Kwa upande wake kijana mwengine aliyetambulika kwa Jina Moja la Juma naye alionekana kupata wasiwasi kuhusu upatikanaji wa ajira hiyo kwenye jeshi hilo ambalo ni la muhimu katika Taifa letu.

        “Jamani hivi mimi sina bahati na soko hili la Ajira la Tanzania nimezunguka na vyeti vyangu zaidi ya miaka miwili nakosa kazi hivi haka “kadegree” yaani Shahada yangu ina nini jamani mbona nateseka hivi”alisema Juma
Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kupata ukweli kutoka kwa maofisa hao wa Jeshi la Uhamiaji kuhusu shutuma hizo,ambapo alijitokeza Ofisa mmoja ambaye akutaka kutaja jina lake kwa kusema yeye sio Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji.

         “Hatuna Jinsi sisi ndugu mwandishi,kumbukeni pia na sisi binadamu  hebu wewe ungekuwa kuwa sisi ungefanyaje,maana watu ni wengi sana nchi hii hawana Ajira,na tumefanya kazi kubwa sana kuwapunguza”

        “Kwani watu waliomba zaidi ya Laki mbili,tena tumewapunguza mpaka wakamebaki kiasi ambacho tunaweza kukimudu,na hawa wenyewe unaowaona tumewagawa kimakundi wengine wamekuja leo
     
       “Ijumaa”na wengine tumewapangia tarehe 16 mwezi huu,hali ni mbaya sasa kaka Ajira hakuna watu wanachanganyikiwa tu hao”alisema ofisa huyo
Mwandishi alipotaka kujua nafasi hizo ambazo idara hiyo ni   watu wangapi,ofisa huyo alisema waitaji watu 250.
Uchunguzi wa Mwandishi wa Mtandao huu,umebaini idadi ya watu waliofika tu kwenye usahili wa kwanza ni zaidi ya elfu ishirini huku kukiwa na hatua nyingine ya usahili itakayofanyika jumatatu ijayo,ambayo nayo itakuwa na watu wengi zaidi ya hiyo.

        Vijana hao waliojitokeza kwenye usahili huo, ni miongoni  mwa waliomaliza  kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini,ambao wanye ngazi ya elimu kwaanzia Diploma hadi shaada ya pili .

      Naye msomi na mchambuzi wa Masuala ya Kisaisa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma,Seiph Yahaya alisema kwa sasa Serikali inahaja ya kutafakali kauli ya aliyoisema Edward Lowassa,kuhusu kauli yake ya ukosefu wa Ajira kwa vijana.

      “Kikuweli mimi nakwambia hili ni Bomu tu linalosubili kupasuka mda wowote tu,sahivi hali ni mbaya sana hususani linapofikia suala la Ajira inakuwa balaa na yote haya ndugu yangu ni Makosa yalifanywa na Serikali hii,haiwezekani wamalize Viwanda vyote kwa kuviua”


     “utategemea nini sasa,kama serikali ingewekeza kwenye viwanda vyandani sidhani tatizo lingekuwa kubwa kama sasa kama hivi ilivyokuwa kubwa,na lazima hili litakuwa Bomu tu”alisema Seiph Yahaya   

No comments: