Tuesday, June 17, 2014

NEWS ALERT: MUME WA FROLA MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI kWA KESI YA UBAKAJI



 Na  Mwene Said 

    MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha (pichani) amefikishwa katika   Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili  ikiwemo ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

    Wakiliwa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini  Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa  nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

 Hata  hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo . Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana. Hakimu
Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja  awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini  hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.


Mshtakiwa   alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.

No comments: