KATIKA kuonyesha ubora kwa Watanzania
mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika
kuboreshaji sekta hiyo, baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha
kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.
Cheti hicho kilikabidhiwa jijini
Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa
kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.
Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma,
alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti
mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hicho kinachoipa
heshima Tanzania.
Profesa Nkoma, alieleza kuwa umefikia
wakati muhafaka wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ifikapo 2017 ili Shirika
hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu.
“Cheti tulichopata ni ISO 900:2008
kimetokana na ushirikiano tulioana miongoni mwa wafanyakazi wote na sio
mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti
hichi ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.
Aidha mkaguzi huyo Andrew Rowe, ilihitaka
TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora ili kuendelea kubaki
na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.
“Inatakiwa kuongeza juhudi katika utoaji
wa huduma ya mawasiliano kwani ni sekta muhimu kwa taifa hasa Tanzania” alitoa
rai Andrew.
Akizungumzia ubora wa cheti hicho,
Mhandisi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Salvatory
Rusimbi, alisema kutokana na viwango bora vya kazi, uongozi bora na matumizi
bora ya rasilimali zinazo tumika kunufaisha utendaji kazi ndio vitu
vilivyochangia kupata cheti hicho.
“Naipongeza TCRA kwani mkaguzi ameona kazi
inayofanywa katika utoaji wa mawasiliano nchini pia utendaji huu utawanufaisha
wateja hivyo inatakiwa kuongeza ushirikiano katika kazi” alisema Rusimbi.
No comments:
Post a Comment