Mkuu wa kitengo cha internent wa TIGO bw DAVID ZACHARIA akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita |
Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania leo
imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya technologia ya HUAWEI ili
kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo ya simu nchini kuweza kupata simu za kisasa "SMARTPHONES " kwa bei nafuu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam muda
mchache uliopita mkuu wa kitengo cha internent wa tigo bw DAVID ZACHARIA
amesema kuwa ushirikiano huo unawapa wateja fursa ya kuweza kumiliki simu aina ya
HUAWEI Y330 kwa bei ya punguzo ya
shilingi 130,000 na HUAWEI Y530 kwa shilingi 195,000 tu.
Ndio aina ya simu ambazo zitakuwa zinauzwa |
Kwa mujibu wa Bw ZACHARIA wanunuzi wa simu hizi
mbili watapata kifurushi cha bure cha thamani ya shilingi 30,000 katika mwezi
wa kwanza baada ya kununua ambapo kifurushi hicho kinajumuisha dakika 600 za
muda wa maongezi,sms 8000,za bure na 1.5 GB za
data za internent.na katika miezi sita inayofuata mteja atakayenunua
kifurushi cha mwezi cha shilingi 15,000 atarudishiwa kiwango sawa na alichonunulia,ambapo
amesema inamaanisha kuwa baada ya baada ya miezi sita
mteja atakuwa amerudishiwa zaidi ya shilingi 120,000.
Akizungumza katika mkutano huo wa waandhishi wa
habari meneja chapa wa kanda ya Africa mashariki na kusini toka HUAWEI AZALEA DU amesema kuwa HUAWEI Y 330 ni simu za kisasa zinazolenga vijana
ambapo kampuni yake inafarijika sana kuwapatia wateja wa tigo fursa ya
kuitumia.
Mwakilishi kutoka HUAWEI akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya TIGO TANZANIA |
Ofa hii inakuja ikiwa ni miezi michache tangu
kampuni ya tigo kutangaza kuwapa wateja wake uwezo wa kutumia FACEBOOK buree
kabisa kwa lugha ya Kiswahili ambapo wateja wake wameonekana kuifurahia sana .
No comments:
Post a Comment