Saturday, June 21, 2014

WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UANDISHI WA HABARI ZA KITAKWIMU YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

 Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
 Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akitoa mada katika warsha hiyo. Kushoto ni Watakwimu, Stephano Cosmas na Hashim Njowele.
 Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
 Mtakwimu, Stephano Cosmas, akitoa mada katika warsha hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
 Maofisa wa Takwimu, Stephano Cosmas na Hashim NNjowele wakisubiri kutoa mada katika warsha hiyo.
  Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke (kushoto), kufungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.Albina Chuwa.
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.
Dotto Mwaibale, Morogoro
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kwa ajili ya kuhamasisha Umma kuhusu umuhimu wa Takwimu.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii, Morice Oyuke mjini Morogoro leo asubuhi wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu.
“Ninyi wanahabari ni muhimu katika masuala ya takwimu hivyo ni vizuri mjifunze jinsi takwimu zinavyoisaidia serikali, wadau wa maendeleo na wadau wa takwimu katika kupanga Sera na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania Bara na mwaka 2020 Tanzania Zanzibar” alisema Oyuke.
Oyuke alitaja mambo mengine wanayopaswa kujifunza ni  Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (Mkukuta) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (Mkuza) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2010/11 mpaka 2015/16 na Malengo ya Melenia (MDGs)
Alisema eneo jingine watakalofundishwa ni kuhusu Pato la Taifa na jinsi linavyokokotolewa na bei za ajira, takwimu za jamii na umuhimu wake.
Dk.Chuwa alisema vyombo vya habari vinajukumu la kutoa taarifa sahihi zilizo rasmi ambazo zinazalishwa na tafiti mbalimbali nchini ili ziwafikie wadau wote nchini bila ya kupoteza maana.

No comments: