Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam limewakamata majambazi sugu wanane ambao wanatuhumiwa kwa
makosa mbalimbali ya ujambazi jijini Dar es Salaam. Katika uhalifu huu
majambazi hao walisababisha vifo, majeraha, wizi wa mali na fedha taslimu.
Katika matukio hayo walitumia silaha za moto ikiwa ni paoja na bunduki aina ya
SMG, Bastola na vifaa mbalimbali vya uvunjaji ikiwa ni pamoja na baruti.
Majambazi hao
wamekamatwa kutokana na oparesheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam baada
ya kifo cha Mtawa wa Kanisa Katoriki Sista CLESENCIA D/O KAPURI, Miaka 50,
Mhasibu wa Parokia ya Makoka, kilichotokea tarehe 23/06/2014 eneo l Ubungo
Kibangu.
Wawili kati ya
watuhumiwa hao nane, wamehusishwa moja kwa moja na tukio la kuuawa kwa Mtawa
huyo ambao wa kwanza ni MANASE S/OGENYEKA @ MJESHI, miaka 35, Mkazi wa Tabata
Chang’ombe, ambaye pia ni mwendesha bodaboda. Wa pili ni HAMIS S/O ISMAIL,
SHABAN @ CARLOS, Mfanyabiashara, Mkazi wa Magomeni Mwembechai.
Majambazi hawa wawili
hatari licha ya kuhusishwa na tukio la kifo cha Mtawa na kupora million
ishirini (20,000,000/=), pia walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za
tukio la uporaji wa Benki ya BARCRAYS tawi la Kinindoni lililotokea tarehe
…………………. Ambapo mamillioni ya fedha yaliibwa kabla na baada ya tukio la
uporaji. Jambazi MANASE S/OGENYEKA @ MJESHI, ndiye aliyeendesha pikipiki
akimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamillioni ya fedha na kutoroka nazo
wakati ambapo jambazi HAMIS S/O ISMAIL, SHABAN @ CARLOS, ndiye aliyekuwa
kiongozi katika tukio hilo.
Jeshi la Polisi bado
linawatafuta watuhumiwa wengine wawili katika tukio la Mtawa na jambazi mmoja
kwa jina maarufu la LEONARD S/O MOLLEL katika tukio la Barcrays Bank ambaye
alitangazwa na kisha picha zake kutolwa katika vyombo mbalimbali vua habari.
Majambazi hao wawili
pia wameshirikiana na wenzao sita kama ifuatavyo:
·
MICHAEL S/O ROMAN
MUSHI @ MASAWE, Miaka 50, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Makabe – Kimara.
·
SADICK S/O MOHAMED
KISIA, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kizuiani.
·
ELIBARIKI S/O ELIAH
MAKUMBA, Miaka 30, Mkazi wa Buguruni Madenge.
·
NURDINI S/O SULEIMAN,
Miaka 40, Mkazi wa Buguruni Madenge.
·
MRUMI S/O HAMAD SALEHE
@ Chai Bora, Miaka 38, Mkazi wa Kigogo Fresh.
Licha ya kushiriki
katika matukio mbalimbali watuhumiwa hawa watatu ELIBARIKI S/O ELIAH MAKUMBA,
NURDINI S/O SULEIMAN, na MRUMI S/O HAMAD SALEHE @ Chai Bora, walikamatwa baada
ya kutumia mbinu ya hati bandia wakiwa wananomba kazi katika kampuni binafsi ya
ulinzi iitwayo “INSTANT SECURITY SERVICES” iliyopo mtaa wa Msasani Makangira.
Majambazi hawa walikuwa wanaomba kazi ya ulinzi katika kampuni hiyo ili baadye
waweze kutenda uhalifu wao wenyewe au wawaruhusu wanamtandao wenzao waweze
kutenda uhalifu kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment