Thursday, July 31, 2014

HALI YA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA BADO TETE,LHRC WATOA REPORT YAO YA NUSU MWAKA,JIONEE HAPA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo kuhusu Repoti hiyo
          Kituo cha sheria na haki za binadamu tanzania LHRC leo kimetoa report yake ya nusu mwaka ya haki za binadamu report ambayo inaonyesha  bado hali ya haki za binadamu kwa Tanzania ni tete na jitihada za serikali bado zinahitajika kujinasua na hali hiyo.
         
       Katika repoti  hiyo ya miezi sita tu inaonyesha kuwa watu 320 wameuawa kwa imani  za kishirikina ukilinganisha na watu 303 waliouawa mwaka jana pamoja na  matukio 473 yameripotiwa kuuawa kwa watu na wananchi wanaojiita wenye hasira kali ukilinganisha na matukio 597 ya mwaka jana ambapo takwimu inaonyesha kupungua,
Mwanasheria kutoka LHRC,  MLOWE  akifafanua yaliyomo ndani ya  Report hiyo
Aidha report hiyo inaonyesha matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yameanza kuongezaka kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya.
           
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa maswala mengi kama mauaji ya vikongwe,mauaji ya walemavu wa ngozi,migogoro ya ardhi,ajali za barabarani,wananchi kujichukulia sheria mkononi,na mambo mengine kama hayo bado ni changamoto kubwa kwa nchi ya tanzania ambapo amesema ni lazima serikali akazie mkazo maswala hayo.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini
Bi HELLEN amesema kuwa ili kudhibiti hali hii ni lazima kwa elimu ya haki za binadamu irudishwe kwenye mfumo wa elimu rasmi wanchi,pamoja na serikali kutunga sheria inayolinda haki za mtoa taarifa ili kuweza kupata ushirikiano wa wananchi katika mapano dhidi ya vitendo viovu.

     Aidha ameitaka serikali kuboresha mifumo ya utoaji haki ikiwa ni pamoja na mahakama na mabaraza mbalimbali ya utatuzi wa migogoro ili kukuza dhana ya utawala wa kisheria nchini
Report hiyo imetoka leo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake wa Africa inayoadhimishwa kote Africa.

No comments: