Tuesday, July 29, 2014

HUZUNI KUBWA--HALI YA MSANII BAHATI BUKUKU SIO NZURI,MAOMBI YAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YAKE


                                                     Na Karoli Vinsent

HALI ya Msanii Hodari wa Nyimbo za Injili Nchini Tanzania Bahati Bukuku inazidi kuwa mbaya,sasa kinachoitajika ni Maombi na sala  kutoka kwa Watanzania ndio itakayoweza kumwokoa Msanii huyo wa Injili,Mtadano umeambiwa.
       
  Bahati Bukuku,ambaye alipata ajali mbaya ya Gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili  iliyopita kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa  Mkoani Dodoma m,ajira ya saa tisa usiku wakati alipokuwa anakwenda Mkoani Shinyanga,Kahama kwenye mkutano wa Injili ambapo ajali ndiyo iliomleta matatizo makubwa.
          
  Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao kwa Njia  ya Simu Rafiki wa karibu wa bahati Bukuku,ambaye akutaka kutaja Jina kwenye Mtandao huu kwa kusema yeye sio msemaji wa Familiya Bukuku alisema kwa sasa hali ya Bahati bukuku inazidi kuwa mbaya sana na  sasa kinachoitajika ni sala na Maombi tu.

      “Da leo nimeoka kumwangalia Hospitali yaani da hali ya Rafiki yangu Bahati Bukuku ni mbaya sana na kinachoitajika sahivi ni maombi tu,maana ukimwangalia mpaka unapatwa na huruma sana tena unapata maswali ya kujiuliza huyo ndio msanii mwenye afya tele juzi tu?”alihoji mpashaji huyo Habari
 Mwandishi wa Mtanda huu alipomtaka Rafiki huyo ataje kitu gani kinachopelea hali yake bahati bukuku kuwa mbaya,
       
   “Bahati ameumia sana kwenye kiuno na ukimwangalia utajua Kiuno kimevunjika na sehemu zengine ikiwemo Shingo hawezi kukaa wala kutembea yeye amekuwa mtu wa Kulala tu,na kinachoitajika sahivi ni sara tu sio kitu kengine maana uwezekano wa kupona ni mdogo sana”alisema mtoa huyo taarifa.
      
          Msanii Bahati Bukuku,ambaye anatamba nyimbo kadhaa ikiwemo Dunia haina Huruma,Maamuzi pamoja na Majaribu ambapo katika Ajari hiyo Dereva wa Gari aliyokuwa anasafilia haina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili T 7945 Edsoni Mwakabungu “EDY” Miaka 31 ambaye ameumia Vibaya sana na Vidole na pia hawezi kutembea kabisa
          
       Watu wengine waliokuwemo kwenye Ajari hiyo  ni Wacheza shoo wa Bahati Bukuku Franki Muha (20) na mwenzake kwa Jina halikupatikana mala moja.
      
     Naye Bahati Bukuku alinikuliwa na Mtandao mmoja wa Habari huku akisema kwa shida sana alisema kwa sasa hali yake ni mbaya sana na kuwataka watanzania kumwombea ili apone na aje kuendelea na kazi yake ya kuendeza Injiri.
         
    Msanii huyo ambaye ni Mwenyeji Mkoani Mbeya kwa sasa bado amelazwa Hospitari ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam .

No comments: