Sunday, July 6, 2014

KIONGOZI WA CHADEMA ASHAMBULIWA KIGOMA

???????????????????????????????Makamu mwenyekiti Uenezi CHADEMA kanda ya Magharibi Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital yaMaweni)baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana(Picha na Editha Karlo)

WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi kanda ya Magaharibi Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma(Maweni).

Tukio hilo limetokea jana majira ya  saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea eneo la Mwanga kuangalia mechi za  kombe la Dunia.
Akiongea na mtandao huu wodini nalipolazwa juu ya tukio hilo   kiongozi huyo alisema kuwa alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla walitokea wanne,mmoja alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine wakimshambulia kwa kisu,nyembe na ubao.
Alisema mbali ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi iliyokuwa mfukoni.
Baada ya watu hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospital kwaajili ya matibabu.
 Makamu Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya kisiasa kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe wa fupi wa maneno ya vitisho  kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni wananchama wa chama kipya cha ACT.
”Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha”alisema Kashai

No comments: