.

siasa na maajabu yake--TAZAMA HAPA TUKIO LA AINA YAKE SHINYANGA,MADIWANI WA CHADEMA WALIOHAMIA CCM,WARUDI CHADEMA TENA

Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Hali ilikuwa tete,ngumi zikanukia-kulia ni mmoja wa viongozi wa chadema katika manispaa ya Shinyanga akikabiliana na wanachama wa chadema waliotaka kuleta vurugu uwanjani hapoWananchi wakiwa na Hasira kuona madiwani waliowaita wasaliti wakirudi chadema tena_Hapa ni katika viwaja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako  kumefanyika mkutano wa aina yake ambao pengine unaweza kuuita mkutano wa kihistoria,mkutano ambao uliandaliwa na viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa mashariki wakiongozwa na mbunge wa Maswa mashariki Sylivester Kasulumbayi.Katika mkutano huo wale madiwani wa Chadema ambao mwezi Februari mwaka huu,walijiuzulu na kuhamia CCM,Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo na Sebastian Peter kata ya Ngokolo,leo wameomba radhi na kurudi CHADEMA. Walisema waliahidiwa na viongozi wa juu wa ccm akiwemo Nape Nauye,Mwigulu Nchemba,Ridhiwani Kikwete,Steven Masele n.k kuwa wahame Chadema waende CCM ili baadaye wajiunge na ACT ili waiimarishe lakini wameshindwa kutofautisha ccm na ACT hivyo kuamua kurudi chadema kwani ndiyo chama imara.Walisema waliambia huwezi kuwa ACT ucpitie CCM.Ikumbukwe kuwa madiwani hao walihamia CCM kwa mbwembwe nyingi wakidai CHADEMA haifai kinaendekeza ubinafsi,ukabila n.k,ikafikia hatua wakaitwamadiwani mizigo.

Waliletwa na pikipiki kwenye mkutano_Aliyevaa nguo ya kijani(CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano wa Chadema leo jioni,baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen Masele,Nape Nauye, Habib Machange na viongozi wengine wengi ndani na nje ya chadema na CCM,na kueleza kuwa ccm hawana lolote badala ya kulaghai watu kwa kutumia pesa.

Kijani peke yao_Kulia ni Sebastian Peter diwani wa Ngokolo akiwasili katika eneo la mkutano,leo.Katika hali ya kushangaza baada ya madiwani hao kuwasili kwenye mkutano vurugu za hapa na pale zilitawala takribani dakika 15 lakini baadaye hali ilikuwa shwari baada ya mbunge Kasulumbayi kutoka jimbo la Maswa mashariki kutumia akili na nguvu nyingi kutuliza wanachama wa Chadema waliokuwa na hasira na kutopendezwa na kitendo cha kuwaleta wasaliti wa chama eneo hilo

 Madiwani wasaliti kama wanavyoitwa   hivi sasa hapa Shinyanga,wakiwa na nguo za CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la mkutano jioni ya leo.

Mkutano huo ni wa aina yake umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga,kila mtu akiwa na lake moyoni,wengine wakisema CHADEMA wawapige chini madiwani hao,wengine wakisema wasamehewe kwani mungu karudisha kondoo wake waliopotea.

Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi.

Wengine walilia kwa hasira_Wananchi wakiwa hawaamini kilichokuwa kinaendelea uwanjani hapo,matusi yalitawala.Picha na Kadama 

Ilikuwa siyo hali ya kawaida-wengi walibaki midomo wazi,walipigwa na hali ya mshangao,wenye kushika viuno haya,wenye kununa haya,wenye kutukana haya,wenye kusema bora liende nao walikuwepo,wenye kuisikitikia chadema kwa kupokea watu wanafiki na wasaliti haya,wenye kukumbuka mbwembwe za CCM wakati wa kuwanyakua madiwani hao wa chadema tena katika eneo hill hilo nao hawakukosekana.

Madiwani hao wawili wakiwa jukwaani tayari kuzungumza na wananchi wa Shinyanga,kulia ni mbunge Kasulumbayi akiwakaribisha.

Tunavua uccm-Kama walivyovua magwanda ya CHADEMA mbele ya Nape Nauye wa CCM,leo madiwani hao wamevua pia nguo za CCM,lakini tofauti na kipndi kile leo hawakuchoma moto nguo.


Mbunge Kasulumbayi akiwa ameshikiria nguo za CCM za Sebastian Peter na Zacharia Mfuko,akasema CHADEMA haina chuki na ccm hivyo kusisitiza kuwa kamwe hawawezi kuchoma moto nguo hizo ila yeyote anayezipenda basi akachukue. 

Kushoto ni Zacharia Mfuko baada ya kuvua nguo za CCM,akiwaomba msamaha wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumla.Alisema walihadaiwa na CCM,kamwe hatarudia kosa na kuongeza kuwa hata nguvu za giza/dawa/uchawi zilitumika kuwachanganya akili ili waidharau chadema lakini sasa wamegundua ujanja wa ccm na kuwatahadhalisha wengine wenye nia ya kwenda CCM waache kwani hakifai.

Kushoto ni Sebastian Peter baada ya kuvua nguo za CCM,akizungumza jukwaani ambapo aliwataja viongozi wa ccm walioshiriki katika mchakato mzima wa kuwahadaa kuwa ni mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele,Ridhiwani Kikwete,Habibu Machange,Mwigulu Nchemba,(Emmanuel Kidenya,Zenna Musa Gulam na mwingine aliyejulikana kwa jina la moja Eliza- hawa ni makada wa Chadema).Leo wamerusha kombora kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa ccm  kuwa walikuwa wameahidi kuwapa shilingi milioni 50 madiwani hao ili wasiende kwenye mkutano wa leo.

......Hiki ninachokiona sasa hivi ni ndoto,mazingaombwe au ndiyo kile waungwana wanachosema kuwa siasa ni mchezo mchafu......

Katikati ni diwani wa viti maalum kata ya Masekelo(anayotoka Zacharia Mfuko) bi Zainabu Kheri akitafakari jambo kwenye eneo la mkutano

Baada ya kutangaza kurudi tena chadema na kukaribishwa tena kwa mikono miwili madiwani hao wakiwa wamekaa na viongozi wa chadema,kabla ya kutoroshwa kimya kimya eneo la mkutano wakati mkutano ukiendelea....Hofu ni usalama wa maisha ya madiwani hao.

Wananchi wakishangaa namna madiwani hao walivyotoroshwa uwanjani hapo na gari ambayo haikujulikana ilitokea wapi.

Hiyo ndiyo gari iliyotumika kuwatorosha madiwani waliohamia tena Chadema baada ya kudai kushindwa majukumu waliyopewa na viongozi wa ccm ikiwemo kutekeleza mauaji ya baadhi viongozi wa CHADEMA akiwemo Dr Slaa .Ikumbukwe pia kuwa wakati wanahamia ccm madiwani hao waliwatuhumu viongozi wa juu wa chadema kuwa walitaka kumuua mbunge wa shinyanga mjini wa ccm Steven Masele.

Mbunge Kasulumbayi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwakaribisha madiwani hao na kwamba sasa ni madiwani tena kwa sababu wakati wanajiuzulu hawakufuata taratibu kama vile kwenda mahakamani,kuwasilisha vitambulisho vya udiwani na vyeti vyao vya ushindi na kuwashangaa CCM kwani hawako makini kwa sababu hawakujua kuwa watu waliowachukua ni wajanja kwa vile hata kadi za ccm hawakuchukua na wamefanikiwa kujua siri za ccm na mipango yao katika kuimaliza CHADEMA na kamwe hawataweza.

Katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga ,ambaye pia ni mwenyekiti wa wazee chadema taifa Nyangaki Shilungushela maarufu kama mzee wa utaratibu akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kilichotokea leo ni mchezo wa siasa kwani katika siasa hakuna uadui wala urafiki leo yanatokea haya kesho mengine ni utaratibu tu

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga bi Siri Yasin akifunga mkutano leo jioni.]
Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Habari zilizoufikia mtandao huu wa malunde1 blog ni kwamba wale madiwani wa chadema Sebastian Peter na Zacharia Mfuko katika manispaa ya Shinyanga waliojiuzulu mwanzoni mwa mwaka huu na kujiunga rasmi na CCM, sasa hali ni tete,inadaiwa kuwa leo watatangaza uamuzi mgumu wa kuhamia tena CHADEMA katika mkutano wa hadhara eneo la viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane.

Sebastian Peter na Zacharia Mfuko wakihamia ccm walidiriki kuchoma hadi nguo za Chadema hadharani
Madiwani waliohama chadema shinyanga kwa hila za MM na Nape waeleza vyanzo vya mapato ya ACT, waomba radhi warejeshwe chadema


Madiwani wawili waliohamia CCM kutoka CHADEMA, katika kata za Ngokolo na Masekelo, Shinyanga, Sebastian Peter na Zacharia Mfuko, wameibuka na kusema wanajutia uamuzi wao, na sasa wanafanya jitihada za kuomba warejeshewe uanachama wa CHADEMA baada ya kukerwa na hila za CCM na ACT.


 
Madiwani hao wanadai kuwa walihamia CCM kwa muda -kwani waliambiwa kuwa ACT kitakapokuwa kimepata usajili wa kudumu wangejiunga nacho ili kuimarisha upinzani nchini.

Madiwani hao walijiunga na CCM Februari mwaka huu na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye. Baadaye, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa alikituhumu CCM kwa mchezo mchafu.

“Tulishawishiwa kuhamia CCM kwa muda kwa lengo la kuhamia ACT ili kikipata usajili wa kudumu tuhamie huko pamoja na baadhi ya wanachama wa CCM.

“Tuliambiwa tufanye siasa za harakati, lakini tulichobaini ni kuwa tangu tukubali mawazo hayo ya viongozi wa ACT tukijua tunaimarisha upinzani imekuwa tofauti. Mkakati huo ulianza kuratibiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Abbakari Gulam ambaye ni mtoto wa Meya wa Shinyanga, wakiwa na Habib Mchange, kisha tuliona mkakati unatekelezwa na mbunge wa Shinyanga mjini, Stephen Masele, Nape Nauye, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba na Ridhiwani Kikwete,” walisema katika taarifa yao mbele ya waandishi wa habari jijini Mwanza.

Wakisimulia mkakati huo walisema walifikishwa Tinde na kiongozi huyo wa UVCCM kisha wakiwa huko walipigiwa simu na Stephen Masele na kuzungumza Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyewahakikishia kuwa baada ya kuondoka CHADEMA watajiunga na ACT ili iwawezeshe kupata nafasi za uongozi wa kitaifa katika chama hicho kipya, pamoja na kupatiwa kitita kikubwa cha fedha.

Chanzo chetu cha habari kutoka Shinyanga kimeelezwa kuwa baada ya kuhamia walipatiwa kiasi kikubwa cha pesa bandia, na katika kitita hicho waliambulia laki mbili ndio zilikuwa halali, pesa hizo zimetajwa kuwa zilikuwa ziwe milioni kumi na mbili lakini bada ya kuhesabu zilipatikana halali laki mbili tu, na zinadaiwa kutolewana na msaidizi wa Masele akiwa na Mchange katika hoteli ya Karena iliyopo Shinyanga, kabla ya madiwani hao kuondolewa na gari hadi Mwanza na kusafiri kwa ndege hadi Dar es Salaam kwa maelekezo ya Nape.

Tamko hilo linaongeza kuwa “kwa kipindi chote cha kudanganywa tulidhani Zitto anaonewa, hivyo tukaamua kujiunga na Chama chake ambacho alituhakikishia lakini tumebani kuwa ACT na CCM hawana tofauti, mikakati inatengenezwa na ACT ila watekelezaji ni CCM, baada ya kubaini ghiliba hizi tumeshindwa tumetafakari kuwa hata barua zetu tuliandika zikiwa na makosa ya kikanuni hivyo sasa tumemwandikia tena Meya kumuuliza ni kwanini hajatualika kwenye vikao viwili kwa kuwa tulikuwa hatujajiuzulu kisheria.

“Ili mtu kujiuzulu udiwani, kanuni zinasema kuwa diwani anaandika barua kwa Meya, unaambatanisha na kitambulisho cha udiwani, na hati ya ushindi ya udiwani ambayo hatujawapa wala vitambulisho vyetu, tulichokifanya ni kama kuandikiana barua za kawaida tu, na mtu kutangaza kujiunga na Chama kiingine bila kuchukua kadi yao sisi sio wanachama wao na kwa kuwa Chama chetu hakijachukua hatua zozote dhidi yetu basi tunarejea kwetu upinzani kushindana na CCM,” alisema Sebastian mbele ya waandishi wa habari.

Walisema CCM na ACT waendelee na kamari zao kuhadaa watanzania, “jamaa hao wana umakini kidogo ndio maana hawakubaliani kuwa bado hatujajiuzulu kisheria wakakimbilia kutupeleka jukwaani kushangilia, sasa sisi tunarudi kutumikia wananchi wetu kwani hatujavunja sheria, hatukukiuka kanuni za kujiuzulu furaha ya CCM na ACT ni ya muda tu, tulionda huko tumewabaini.

Kufuatia hali hiyo,madiwani hao waliandika kuwa “tunapenda kuomba radhi viongozi wote wa CHADEMA, wanachama na watanzania wote watusamehe, watupokee tukapambane kufanya kazi ya siasa za upinzani wa kweli kuleta ukombozi wa kweli kwa nchi yetu, tulichokiona huku tumekijua, tunawatahahadharisha wengine wakionga inafaa wajiunge huko kwa hasara yao ya maisha yao kisiasa na kufanya kazi ya kujenga CCM.”

Mkakati huu unaratibiwa na mmoja wa wabunge wa upinzani mwenye mahusiano ya karibu na viongozi wa CCM na serikali anayedaiwa hadi sasa kuifadhili ACT mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kujiimarisha mikoani kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.. 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.