Friday, August 22, 2014

LIVE TOKA DAR ES SALAAM---RITA WAJA NA LENGO BORA KWA WATANZANIA,SASA NI TATHMIN YA MFUMO WA USAJILI,MATUKIO MUHIMU NCHINI-STORY KAMILI IKO HAPA

Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita katia ofisi za RITA jijini Dar es salaam
WAKALA wa Usajili na ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya tasmini ya mfumo wa Usajili,matukio muhimu ya Maisha na ukusanyaji wa Takwimu nchini tanzania.

 Mfumo huo ambao utatumika kuchukua taarifa muhimu za vizazi,vifo na Sababu zake,ndoa  na talaka.

 Akizungumzia Tasmini hiyo, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari Jijini ,Afisa Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Alisema Tasmini hiyo itafanyika kikanda kwa siku kumi na tano (15) kuanzia tarehe 15 Semptemba hadi tarehe 30 mwaka huu na itajumuisha wadau wakubwa wa Masula ya usajili kutoka wizara ,Taasisi,Idara pamoja na Vyuo na wakala Mbalimbali za Serikali.

Waandishi wa habari mbalimbali wakiwa katika mkutano huu ambao umemalizika muda huu jijini Dar es salaam
Ambapo ameongeza kusema Tathmini itafanywa katika ofisi za Maafisa tawala wa Wilaya,Vituo vya Tiba ,Vituo vya Polisi,nyumba vya kutunzia Maiti,makanisa na kwenye Makazi ya Wananchi ambamo matuko hayo utokea.

Saliboko amewataka Watanzania kutoa ushirikiana mkubwa wakati wa Zoezi hili,kwani ndio njia pekee itakayoisaidia Serikali kufanya mipango yake kikaminifu.

   

No comments: