Thursday, August 28, 2014

NI MBOWE TENA CHADEMA

Mwenyekiti wa chama cha demcrasia na maendeleo chadema na mbunge wa jimbo la hai mh FREMAN MBOWE  leo ametangaza rasmi kugombea tena nafasi a uenyekiti wa chama hicho kwa lengo la kuendeleza harakati za chama hicho alizozianzisha.

Hatua hiyo imekuja baada ya wazee wa baraza la wazee chadema na wazee kutoka kigoma  kumwangukia na kumtaka agombee tena huku wakimsifu kuwa amekisaidia sana chama hicho tangu akamate uongozi hivyo ni vyema akaendelea kukiongoza tena chama hicho kwa lengo la kutimiza malengo waliyojiwekea.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho leo jijini dar es salaam MBOWE amesema kuwa amesikia maombi ya wazee hao na yupo tayari kugombea tena nafasi hiyo ya uenyekiti wa chama hicho taifa. huku akiwataka wanachama kuwa na imani na chama chao kwani mapambano bado yanaendelea ya kuwakomboa watanzania.

Aidha MBOWE amesema kuwa wale ambao wanajidanganya kuwa chama hicho kimepungua makali wakae mkao wa kula katika chaguzi zijazo ndio watapata majibu ya mwaswali yao.

Baada ya kukubali ombi ilo wazee hao walimkabidhi mwenyekiti huyo kiasi cha pesa shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kuchukua form ya kugombea tena nafasi hiyo ya juu katika chama hicho.



No comments: