Tuesday, August 26, 2014

SERIKALI YAKABIDHIWA MAGARI NA PIKIPIKI KUTOKA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA UJERUMANI (GLRA) KWA AJILI YA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA



Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (wa pili kushoto), akimkabidhi  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),moja ya ufunguo wa gari kati ya magari manne na pikipiki 20 vyote vikiwa na thamani ya sh.261,105,615, Dar es Salaam leo, zilizotolewa na shirika hilo kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo nchini. Wanashuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo na Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe.
Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe (wa pili kulia), na viongozi wengine wa wizara hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Charles Palanjo, Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Pikipiki zilizotolewa kwa serikali.
Magari yaliyotolewa kwa Serikali.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Dk. Deus Leonard katika hafla hiyo.



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akijaribu kuwasha moja ya magari hayo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid(kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Kitabibu wa Ilala, Dk.Mbarouk Seif.



Dotto Mwaibale

SERIKALI imepokea msaada wa magari manne na pikipiki 20 zenye thamani ya sh. .261,105,615 kutoka Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA) kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.

Akipokea msaada huo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema Tanzania imefikia lengo la kimataifa la kutokomeza ukoma kwa kuwa chini ya mgonjwa mmoja katika watu 10,000 hivyo kufanya ukoma kutokuwa tatizo kubwa la afya nchini.

Alisema pamoja na kupokea msaada huo bado kumekuwa na changamoto ikiwemo za ukosefu wa magari na pikipiki kwa mikoa na wilaya mpya ambapo Serikali kupitia mpango huo unafanya jitihada za kupata vyombo vya usafiri katika mikoa hiyo.

Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitapelekwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Halmashauri za Ilala na Kinondoni ambapo aliomba  vitumika vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

"Napenda kuuwaasa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya vyombo hivi vya usafiri kwa kuhakikisha wale wote watakaokabidhiwa wanavilinda kwa kuvitumia vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa na kwa kufuata taratibu za serikali na si vinginevyo," alionya.

Dk. Rashid alitoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuangalia namna ya kuchangia gharama za matengenezo ya vyombo hivyo ili kuziba pengo la kupungua kwa misaada inayotolewa na wahisani.

No comments: