Tuesday, September 9, 2014

GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAWAMANI,IDARA YA UHAMIAJI WALIVA,SOMA KAULI YAO LEO

Naibu kamishna wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji wa uhamiaji Afande Abbas Irovya akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
 Na Karoli Vinsent
IDARA ya Uhamiaji nchini imelitaka gazeti la Tanzania Daima kupelekea ushahidi wa Madai ya Rushwa waliyoishutumu Idara hiyo.
Kauli hiyo ya Uhamiaji nchini inakuja siku moja kupita baada ya Gazeti la Tanzania Daima toleo la jumapili tarehe 7 mwezi huu lenye kichwa kikubwa cha Habari “Ufisadi uhamiaji”ambapo toleo hilo lilisema viongozi wa idara ya uhamiaji wamepokea rushwa ya sh milioni 2  kwa watu kila mtu aliyepewa ajira kwenye idara hiyo na kusema katika watu 200 waliopewa ajira Idarani hapo walitoa pesa hizo ambapo jumla ya fedha zote inafikia Bilioni 2.1
.
Toleo ambalo linalalamikiwa na uhamiaji
Akikanusha taarifa hiyo leo Jijini Dar Es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari, Naibu kamishna wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji  Afande Abbas Irovya,ambapo alisema Idara hiyo imesikitishwa sana na taarifa kwenye gazeti hilo kwani taarifa hiyo inalengo la kupotosha Umma na kuichafua idara hiyo nyeti ya nchi,kwani ukweli ni kwamba mwandishi wa Habari hiyo Martin Malera alishindwa kuweka ushahidi wa moja kwa moja


“Habari kwenye Gazeti la Tanzania Daima toleo la jumapili tarehe 7 mwaka huu imetusikitisha sana kwani habari haina ukweli wowote tena inamalengo ya kutuchafua tu,kwasababu mwandishi wa habari hiyo ameshindwa kuweka hata ushahidi wa moja kwa moja juu ya hao vigogo anaosema kwamba wamechukua rushwa ya Bilioni 2.1 zaidi ya kusema ni kwa mujibu ya vyanzo vyetu,tena mbaya zaidi ameshindwa hata kutufwata sisi watu wa uhamiaji ili kupata ukweli yeye kaishia kuandika Habari ambayo haina ukweli “alisema Irovya  

Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
I rovya alizidi kusema idara hiyo inamtaka mwandishi wa Gazeti hilo apeleke Majina ya hao vigogo wa uhamiaji ambao anaowashutumu ili idara hiyo iwachukulie hatua kali za kisheria kwani kufanya hivyo kutaweza  kuijenga idara hiyo kwa Wananchi,
Aidha Irovya aliwataka Waandishi  wa Habari nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Weledi mkubwa sana ili taarifa zao ziweze kuleta manufaa kwa jamii,
    Huu ni Mwendelezo wa kuzidi kubanwa kwa Gazeti la Tanzania Daima ikumbukwe karipio hili la Idara ya Uhamiaji limekuja siku chache kupita baada ya Ofisi ya Msajili wa Magazeti nchini kuliandikia barua gazeti hilo na kusema liache kuandika habari zenye upotofu kutokana na moja ya matoleo yake yaliyopita yenye kichwa cha Habari “Rais Kikwete ayalamba Matapishi yake” pamoja na “Rais Kikwete anywea”
    Kwa mujibu ya Barua hiyo ililitaka Gazeti hilo kukanusha taarifa  kutokana na habari hiyo Kukwaza Rais Jakaya Kikwete,
    Baada Barua hiyo kulifikia Gazeti hili,ndipo Mhariri wa Gazeti hilo katika toleo la leo tarehe 9 mwezi huu,Katika ukurasa wake wa Kwanza lilikuwa na Kichwa cha Habari “Kumradhi Jakaya Kikwete”


No comments: