KAULI YA BAWACHA KUHUSU RASIMU ILIYOPENDEKEZWA JANA

HALIMA MDEE mwenyekiti wa BAWACHA akizungumza nna wanahabari Jijini  Dar es salaam.
            Baraza la wanawake wa chama cha democrasia na maendeleo chadema BAWACHA wamekuwa wa kwanza kuipinga rasimu ya tatu iliyowasilishwa bungeni jana na kutangaza kuandamana hadi ikuliu ya jiji la dar es salaam kupeleka kilio chao kwa kile walichoitwa kushindwa kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo

           Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa baraza hilo BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa kawe HALIMA MDEE amesema kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama rasimu hiyo ilivyoelekeza bado sio kipaumbele cha wanawake wa Tanzania ila kinachofanyika ni kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.

            Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali mtanzania kwani kuna mambo mengi ambayo yameondolewa yalikuwepo kwenye rasimu ya WARIOBA.

            Wanawake hao wametangaza kufanya maandamano wiki moja ijayo ambayo amekataa kutaja siku rasmi kwa kile alichokisema kuwa bado wanafanya maandalizi ambapo yatakuwa  ya amani ambapo amewataka polisi kuwalinda kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani na utulivu mkubwa yakiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa watanzania wote juu ya mchakato huo wa katiba.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.