Saturday, September 27, 2014

NAJUA WAJUA,NATAKA UJUE ZAIDI KUHUSU HILI

Gari hili limetengenezwa nchini ujerumani na kununuliwa na serikali ya Tanzania tarehe 17,desember 1996,Baba wa taifa mwalimu nyerere alitumia gari hili katika shughuli zake mbalimbali za kitaifa hapa nchini pamoja na shughuli zake binafsi hususani katika mikoa ya Dar es salaam na pwanibaada ya kustaafu urais.MERCEDEZ BENZ e300 ndio gari la mwisho kutumiwa na baba wa taifa kipindi cha uhai wake ,gari hili alitumia mara ya mwisho kabisa tarehe 31,augost 1999 kutoka nyumbani kwake msasani kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa malimu julius nyerere kwa safari ya kwenda london ambapo alikwenda kwa matibabu  ambapo hakurudi tena akiwa hai alifariki huko london,

Gari aina ya AUSTIN MORRIS A40 imetangenezwa nchini  uingereza kati ya mwaka 1940-1950,gari hii ni ya awali kutumiwa na baba wa taifa na rais wa kwanza wa tanzania hayati MWALIMU NYERERE kuanzaia mwaka 1955-1960 katika nshughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU,gari hili liliendeshwa na dereva maalum maremu SAID TANU.

No comments: