Tuesday, September 2, 2014

TIGO IMETISHA--SASA WATEJA WA TIGO PESA WANAGAIWA FAIDA ,SOMA UONE

Meneja mkuu wa Tigo Tanzania DIEGO GUTIERREZ akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya huduma hiyo  
 Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania leo imetangaza kutoa gawio la kiasi cha shilingi billion 14.25 sawa na dola za kimarekani 8.7 lililolimbikizwa katika account  yake ya fedha ya tigo pesa kwa ajili ya wateja wake.hii inafanya kampuni hiyo kuwa mtandao wa kwanza wa simu duniani kutoa gawio la fedha kutokana na huduma ya kutuma na kutoa fedha.
       Acount ya mfuko wa fedha wa tigo pesa TIGO PESA TRUST ACCOUNT ni account ambayo fedha za tigo pesa zinakusanywa na kuhifadhiwa toka huduma ya tigo pesa ilipoanza miaka minne iliyopita.Kwa sasa TIGO  ipo tayari kutoa gawio la fedha hizo ambazo zilikuwa zinazaa faida baada ya kuridhiwa na benk kuu ya Tanzania BOT kwa barua rasmi ya kutokuwa na pingamizi iliyopokelewa julai mwaka huu.
       Akizungumza na wanahabari leo meneja mkuu wa TIGO Tanzania  DIEGO GUTIERREZ amesema kuwa gawio hilo la faida litawanufaisha wateja wote wa tigo wakiwemo mawakala wakuu mawakala wa reja reja na mteja mmoja mmoja mtumiaji wa tigo pesa.
Amesema kuwa kwa miaka mitatu na nusu sasa mfuko wa fedha wa tigo pesa ulikuwa ukikusanya faida  ya kiwango cha asilimia 5 hadi 12 na mpaka juni mwaka huu faida hiyo imefikia shilingi billion 14.25 na kuongeza kuwa lengo ni kuwapatia wadau wa tigo fursa ya kupata faida kutokana na kiasi cha fedha walichoweza kukiweka katika account zao za tigo pesa.
Aidha amesema kuwa wastani wa faida ambayo mteja yeyote ataweza kupata inatofautiana na wastani wa fedha ambayo ataweza kubaki nayo kwenye account yake ya tigo pesa kwa siku kwa hiyo viwango vinatofautiana kati ya wakala mkuu,wakala wa rejareja na mteja mmoja mmoja.


Gawio hilo litawanufaisha zaidi ya wateja million 3.5 wa tigo pesa nchini wakiwemo mawakala wakuu,mawakala wa reja reja.

No comments: