Sunday, October 12, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--KURA NYINGINE FEKI ZANZIBAR HII HAPA,JUKATA WASEMA MAZITO

Mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania JUKATA ndugu DEUC KIBAMBA akizungumza na wanahabari muda huu Jijini Dar es salaam
  Exaudi Mtei na Karoli Vinsent

MAPYA yanazidi kuibuka juu ya Hujuma alizofanya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta wakati wa kupata thulithi 2 ya kura kwa upande wa Zanzibar  ili kupitisha Rasimu iliyopendekezwa
         Na bunge la Maalum Katiba baada ya Jukwaa la Katiba nchini JUKATA kuibuka na kufichua hujuma nyingine ya Thulithi 2 kwa upande wa Zanzazibar baada ya kubaini kuorodheshwa kwa Mjumbe wa Bunge hilo kutoka Tanzania bara ambaye jina lake limeorodheshwa kwa majina ya wapiga kura kwa upande wa Zanzibar.

Kuibuliwa hujuma hizo za Jukata imekuja siku chache kupita baada ya Chama cha NCCR Mageuzi kubaini kuorodheshwa kwa mjumbe kutoka chama hicho kwa upande wa Zanzibar kupiga kura ya ndio wakati hakushiriki vikao vya bunge maalum la katiba.
Wanahabari mbalimbali Tanzania wakiwa wanasikiliza kwa makini      
Mapya hayo juu Hujuma ya Theluthi 2 yameibuliwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Nchini JUKATA Deus Kibamba wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibamba akizungumza kwa uchungu  kwamba wamechunguza wameibani kuorodheshwa Zakhia Meghji ambaye ni Mjumbe kutoka Tanzania bara kupiga kura ya ndio kwa upande wa Zanzibar.


“Jukwaa la katiba limebaini kuwapo kwa mjumbe mwingine feki kwa upande wa Zanzibar Zakhia Meghji ambaye   ameorodheshwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge la Maalum la katiba namba 149  kwamba ni mjumbe wa Zanzibar na kapiga kura ya ndio wakati yeye anajulikana wazi ni mjumbe wa Tanzania bara wakati  mjumbe huyo kupitia Gazeti la Serikali la mwezi julai lilimtaja Zakhia Meghji kuwa ni mjumbe Tanzania bara inakuweje leo tena wakati wa kupiga kura  atambulike kwamba ni  mjumbe wa Zanzibar yote haya ni kufanya hujuma ili kupata thelusi 2“Alisema Kibamba .
           
   Kibamba alizidi kusema kwa hali hiyo ya kufanya uchakachuaji kwenye kupiga kura upande wa Zanzibar ni wazi basi thelusi 2 haikupatikana bali alichafanya Sitta na wenzake ni kuwadanganya watanzania na kusema kuwa Jukwaa la katiba limebaini tayari kumekuwa na dosari sana wakati wa kupata theluthi 2 na hizo kura mbili ambazo amesema Sitta kwamba ndio zimepitisha katiba ni uongo.

 Aliongeza kuwa kwa sasa Jukwaa la katiba nchini limeipa kazi kampuni moja ilitobobea kufanya uchunguzi wa kwenye kura za wajumbe  kwa upande wa Zanzibar na wakibaini kwamba kuna kura nyingine feki basi watachukua hatua kali.
    
    Aidha,Kibamba alisema JUKATA wamesikitishwa sana  na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuyazika kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi kwa kitendo cha kuondoa Mamlaka na madaraka ya Wananchi,maadili na mikio ya uongozi na utashi kwa umma na kuzidi kuendelea Tanganyika kuvaa koti la Muungano.
           
Ambapo alisema kwa sasa Jukwaa la katiba Linajipanga kusambaza Rasimu ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalum nchi nzima ili wananchi waamue ukweli juu ya katiba.
      Vilevile JUKATA limewataka watanzania kusoma kwa umakini Katiba iliyopendekezwa na bunge iliwaweze kujua ukweli


No comments: