Thursday, October 2, 2014

MIKOPO KWA WANAFUNZI SASA NJIA PANDA--SOMA KAULI YA TAHLISO HAPA

Na Karoli Vinsent

         HUKU ikiwa bado Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB)  ikiwa inasuasua kutaja majina ya Wanafunzi wapya watakaopata Mikopo wa mwaka wa masomo 2014-2015,kutokana na bodi hiyo kusema inauwezo wa kuwapa mikopo wanafunzi 30000 tu kati ya wanafunzi 58,037  waliomba mwaka huu. Kwa madai bodi hiyo imepewa Bajeti ndogo na serikali,

        Nao Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO)imezidi kuibana serikali na kusema haitokubali kusikia wanafunzi wanakosa mkopo na kusema kila mwanafunzi wa anayejiunga elimu ya juu nchini anahaki kupata mgawanyo sawa wa keki ya Taifa.

         
        Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu (TAHLISO) Musa leonard Mdede, wakati wa Mkutano na Waandishi na Habari,ambapo alisema maazimio ya Mkutano mkuu wa Tahliso uliofanyika Chuoni RUCO-Mkoani Iringa,umeitaka Serikali kwamba wanafunzi wote waliomba mkopo katika mwaka huu wamasomo wapewe wote.
      
       “Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kwamba wanafunzi wote waliomba mkopo mwaka huu yaani wanafunzi 58,037 wapewe wote  kama tu kutakuwa wamedahiliwa na tume ya vyuo vikuu  kuingia Elimu ya Juu,hili jambo la dharura na tunaitaka serikali kuhakikisha kufanya hivo kwani wote ni Watanzania wanaostahili mgawanyo sawa wa Keki ya Taifa”alisema Mdee.
     
         Mdee alizidi kusema Jumuiya hiyo imeitaka Bodi ya Mkopo kuacha kutoa Mkopo kwa ubaguzi kutokana na hivi sasa kutoa upendeleo kwa watu wenye kada ya masomo ya Sayansi na Elimu na kuzipa kisogo Taaluma nyingine  kwani bodi kufanya hivyo kutalepelekea Taifa likose wasomi katika masuala mengine ikiwemo Uandishi wa habari,mambo ya Fedha na sheria.
     
        Vilevile Jumuiya imeitaka serikali kupandisha kupandisha mara moja fedha ya kujikimu kwa mwanafunzi wa elimu ya juu toka 7500/kwa siku hadi 15000 na kusema hali ya maisha imependa huku ikizingatiwa garama za vitu viko juu tofautisha na kipindi kile cha nyuma walipopitisha kiasi hicho.
       
       Aidha Mdee aliitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU kusimamia misimamo yake ya mwanzo ambayo ilikuwa inavitaka vyuo Vikuu vyote nchini kutopandisha Ada ya Masomo kutokana na hivi sasa vyuo vya KCMC na St Francis kilichopo Ifakara ambapo vyuo hivyo vimekaidi walaka wa tume ya vyuo vikuu  nchini iliyovita vyuo visipandishe ada za masomo

No comments: