Mmiliki wa kamouni hiyo ambayo imeamua kujenga tren hizo za kisasa nchini kutoka marekani katikati na wenzake wakionyesha picha ya treni hizo ambazo sasa zitafanya kazi jijini dar es salaam |
Serikali ya Tanzania kupitia wizara
ya uchukuzi leo imeingia katika historia nyingine baada ya kusaini mkataba na
kampuni ya SUMOJA kwa ajili ya kujenge tren za kisasa ambazo zitafanya kazi
katika jiji la Dar es salaam tren ambazo kwa sasa zinatumika katika mataifa
yaliyoendelea duniani.
ROBERT SHUMARKER ambaye ndiye kampuni yake iliyojitoa kujenga tren hizo za kisasa jijini Dar es salaam akizungumza na wanahabari muda huu ambapo amesema kuwa kauli mbiu yake ni LEO yani kazi inaanza leo |
Mmiliki wa kampuni hiyo kutoka marekani ambaye
naye pia ni mmarekani akizungumza na wanahabari muda huu makao makuu ya wizara
ya uchukuzi ROBERT SHUMAKER amesema kuwa ameamua kujitolea kulisaidia taifa la Tanzania
kuhakikisha kuwa linapata usafiri wa haraka na makini ambapo amesema kuwa zoezi
la ujenzi wa vituo na njia unanza mara moja kwani hakuna muda wa kupoteza
katika hilo ambapo mradi huo unatarajiwa kugharimu dolla million 35.
Waziri wa uchukuzi nchini Tanzania mh HARISON MWAKYEMBE akizungumza nna wanahabari muda huu jijini dar es salaam juu ya ujio wa treni hizo ambao amesema kuwa ni mkombozi wa foleni za jiji la Dar es salaam |
Aidha waziri wa uchukuzi mh HARISON
MWAKYEMBE amesema kuwa mkataba huo ni matunda ya juhudi za rais wa Tanzania MH
JAKAYA KIKWETE katika kufungua milango ya wawekezaji duniani kuja kuwekeza hapa
Tanzania.ambapo amesema kuwa treni hizo zitaanza kujengwa njia ya pugu na
zinatarajiwa kukamilika ifikapo mwanzoni mwa mwaka kesho.
No comments:
Post a Comment