Tuesday, October 7, 2014

UTAFITI TAMWA--ULEVI HASA WA VIROBA NI JANGA JIPYA KWA VIJANA NCHINI

Na Karoli Vinsent

    Kile kinachoonekana Nguvu kazi ya Taifa inazidi kupungua kutokana na Vijana wengi nchini Kujiingiingiza kwenye tabia unywaji pombe kupita kiasi na Kuacha kufanya Shughuli za Maendeleo na kupeleka vijana kuishia kwenye Umasikini uliopitiliza.
        
         Hayo yamegundulika Leo jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake nchini (TAMWA) ambapo ripoti hiyo ya Utafiti imehusisha kata tatu ikiwemo Makumbushao,Wazo,Tarakea zote zilizopo katika Manispaa ya Kinondoni Jijini dar Es Salaam na lengo la utafiti huo ni kuangalia Jinsi gani Pombe inavyoweza kuleta unyasaji wa Kijinsia.

          
          Akisoma Ripoti hiyo ya Utafiti mbele ya Waandishi wa habari, Mhadhiri Mwandamizi wa Elimu ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Dk Severine kessy,
         
       Alisema utafiti huo umebaini Vijana wengi katika Sehemu hizo wameendekeza unywaji pombe na kuacha kujikita katika masuala ya Maendeleo.
       
        “Utafiti wetu umeangalia Jinsi gani pombe inaweza kuleta athari katika Jamii,  katika kata hizi tatu za Makumbusho,wazo Tarakia,tumegundua Vijana wengi wanatumia vilevi mda wote na Kilevi ambacho wanakitumia sana na Pombe aina ya Kiroba huku wakiaacha kufanya mambo ya Maendeleo”

        “Na kila tulipokwenda katika Kata hizo tumekuta watu wanakunywa Pombe kupita kiasi huku wengine wakitembea nazo mfukoni na hata upatikanaji wa pombe yenyewe zinapatikana kirahisi kwani zipo mita mia tu kutoka kwenye makazi ya watu na matokeo yake unyasaji wa Kijinsia”alisema Dk Kessy.

              Dk Kessy alizidi kusema utafiti huo umebaini  kila Rika yaani kuanzia Vijana mpaka wazee wamekuwa wahanga wa Unywaji pombe.
                 
       

Aidha Dk Kessy alisema Utafiti umegundua sababu ya Vijana wengi kujikita katika Unywaji wa Pombe uliopitiliza na kusema sababu kubwa ni Tatizo la Ajira na msongo wa Mawazo na kuongeza Matizo mengi sana ya Unyanyasaji wa kijinsia umetekona na Unywaji pombe uliopitiliza.
          
           Kwa upande wake  kaimu mkurugenzi wa chama hicho cha habari, Bi. Gladness Munuo Aliitaka Jamii kuachana unywaji Pombe  na kuwataka Vijana wajikite kwenye masuala ya Maendeleo na kuliletea Taifa Maendeleo huku ikizingatiwa Vijana ndio moyo wa Taifa.

No comments: