Thursday, October 16, 2014

WANAFUNZI WALIOKOSA MIKOPO WAANDAMANA HADI WIZARANI KUDAI HAKI YAO

PICHA NA MAKTABA

Na Karoli Vinsent

           KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida leo watendaji wa Wizara ya Elimu makao makuu wameonja joto la jiwe baada ya Mamia ya wanafunzi wapya wa Masomo ya mwaka wa  masomo 2014-2015 kuzizingira ofisi za wizara hiyo  kwa kile wanachodai kunyimwa pesa za chuo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB huku wengi wao wakisema wakitoka kwenye Familia masikini.

           Hayo yameibuka leo kwenye makao makuu ya Wizara ya elimu zilizopo Posta Jijini Dar es Salaam jirani na Ikulu ya Rais,ambapo Mwandishi wa mtandao huu alifika Wizarani hapo majira ya mchana na kukuta mamia ya vijana wakiwa wamezizonga ofisi hizo huko wanalalamika kwa kitendo cha kutopewa mkopo na Serikali.

      
           Mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa Jina moja la John ambaye amechaguliwa Chuo Kikuu cha Mlimani huku akizungumza kwa uchungu sana alisema kwasasa haoni taswira yake ya masomo kutokana na bodi ya Mkopo kumyima pesa za masomo pamoja na za kujikimu.
     
          “Da sijui twenda wapi sisi watoto wa masikini hili taifa mimi ni yatima sina baba wala mama nimesoma kwanzia msingi mapaka kidato cha sita kwenye shule za serikali tena za kata nashangaa leo naingia chuo kikuu nanyimwa mkopo eti bodi wanasema mimi Bajeti aitoshi  sasa sijui nitafanyaje mimi”alisema mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina moja la John.
     
           Naye mwanafunzi mwengine ambaye amechaguliwa Chuo kikuu cha Ualimu cha Duce alisema ameshangaa sana kwa Bodi ya mkopo pamoja na tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU kuwadanganya na pia kuipuuza kauli ya waziri wa Elimu aliyosema kwamba wanafunzi wote waliomba kwenye masomo ya kipaumbele kama walimu wapewe mkopo,badala yake Bodi hiyo imewanyima wanafunzi waliomba kozi za ualimu na kuwapa wanafunzi wengine waliomba masomo yasiyokuwa ya kipaumbele.
     
         Mwengine alisikika akisema“Leo bunge la katiba limetumia mabilioni ya fedha kwenye jambo ambalo wote kwa pamoja tumekuwa mashahidi mchakato ule ulivyokuwa,harafu leo sisi watoto wamasikini tunashindwa kusoma  harafu mabilioni yetu yamepotelea kwenye mchakato wa katiba mpya sijue twende wapi jamani hili taifa hatuoni kama haoa kuna uongozi bora tumechoka”alisema mwanafuzi mwengine
     
           Vilevile wakati wanafunzi hao wakipiga kelele nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu huku wakishinikiza kuonana na Waziri wa Elimu na Mafunzo Shukulu Kawambwa ili kumwelezea hali ilivyo,nje ya eneo hilo kulikuwa tayari Jeshi la polisi lilifika katika eno hilo ambalo lipo jirani na ikulu ili kuweka ulinzi na kuwataka wanafunzi hao waandike majina yote kwenye karatasi na majina hayo yapelekwe kwa Katibu wa Wizara hiyo.
      
       Wakati wanafunzi hao wakiandika majina ofisa Mmoja wa usalama aliyekuwepo ambaye akutaka jina lake litajwe mtandaoni alimwambia mwandishi wa mtandao huu kwamba serikali inaandaa bomu ambalo litakuja kuletea matatizo mbeleni kwani mataifa mengi amani yake imeharibika ilitokana na viongozi kama wa sasa kupuuza

kelele za wananchi na huko kupoteza pesa kwenye mambo ambayo yasiyo ya msingi ikiwemo kwenye Bunge la katiba ambalo mwisho wa siku pesa zimepotea bure.

      
           Juhudi za kuwatafuta viongozi wa Wizara hiyo ili kuzungumzi sakata hilo ziligonga mwamba kutokana viongozi hao kutokuwepo ofisini na simu zao zilipopigwa hazikupatikana.
       
         Kuibuka kwa wanafunzi hao kunakuja siku chacha baada ya Bodi ya Mkopo nchini HESLB kutangaza majina ya wanafunzi waliopata mkopo mwaka wa masomo 2014-2015 ambapo kati ya wanafunzi 57860 waliomba kwa mwaka huu bodi hiyo imewapa wanafunzi 30654 tu na kusema serikali inauwezo wa kuwakopesha wanafunzi hao tu kwakuwa Bajeti iliyotengwa na serikali ni ndogo kuwapa wanafunzi wote mkopo.

No comments: