Sunday, October 26, 2014

YAMETIMIA UKAWA--HII NI HISTORIA YA SIASA ZA TANZANIA,CHEKI PICHA ZA KUSAIN MAKUBALIANO HAPA


Historia kubwa imewekwa muda huu hapa viwanja vya jangwani jijini dar es salaam Tanzania Ambapo vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa muda huu wamesain mkataba ambao unawafanya wao sasa kuungana na kuzungumza lugha moja ya kuhakikisha kuwa wanafika mbali zaidi wakiwa pamoja,umoja huo ambao unaundwa na CHADEMA,CUF,NCCR MAGEUZ pamoja na NLD muda huu wamesaini kwa pamoja makubaliano hayo mbele ya wanachama wao maelfu waliojitokeza katika viwanja hivyo hapa jijini dar es salaam.
Akizungumza na wanachi waliojitokeza hapa katibu mkuu wa chadema aesema kuwa makubaliano hayo sio makubaliano ya vyama na viongozi wakuu bali ni makubaliano ya wanachi wote ambao wanapenda haki na amani ya tanzania.
mtu wangu hapa kuna picha za shuguli hiyo ya kusaini makubaliano hayo na tutazidi kukupa kile kinachojiri hapa uwanja wa jangwani.
Wenyaviti wa vyama hivyo kwa pamoja wakisaini makubaliano hayo ambayo yanawaweka pamoja na kufanya siasa ya Tanzania kuingia katika historia nyingine kubwa na ambayo haijawahi kutokea
Mamia ya wanachama waliojitokeza hapa
Naibu katibu mkuu zanzibar chaderma salum mwalim akizungumza lugha ya tatu.
PICHA NYINGINE ZA TUKIO HILI ZIKO CHINI HAPO


Maalim seif yupo hapa







No comments: