TIGO KUSAIDIA MPANGO WA KUJENGA NA KUTOA VIFAA KWA MAABARA YA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI MTWARA

unnamed
Mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini Bw. Wilman Ndile (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala kwaajili ya ujenzi wa maabara katika wilaya ya Mtwara, kulia kwake niMeneja wa Tigo kanda ya kusini, Bw.Daniel Mainoya na kushoto kwake mkurugenzi wa kampuni ya Proactive Solution, Nestory Phoye.

 ………………………………………………………………………………
Tigo Tanzania leo imetangaza kwamba itasaidia kujenga na kuchangia vifaa katika maabara ya shule za sekondari ambazo zimekwisha jengwa wilayani Mtwara. Mamlaka ya wilaya yanaandaa harambee kubwa siku ya Ijumaa wiki hii kwa ajili kufanikisha jambo hili. 
Akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Kanda ya Mtwara kutoka Tigo Daniel Mainoya alisema kwamba kampuni yake inaamini katika kuwapatia watoto mazingira bora yakusomea, ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuwa wananchi wanaowajibika na kuzalisha ipasavyo. 
“Hii ni muhimu sana hasa hasa katika kujifunza masomo ya sayansi. Ni muhimu kwa watoto wetu kupewa vifaa vinavyotakiwa ili kuweza kupata uelewa si wa kinadharia tu bali wakiuzoefu wa namna ya kujifunza masomo ya sayansi kama Baiolojia, Kemia na Fizikia,” alisema Mainoya. 
Wilaya ya Mtwara, ni moja kati ya wilaya sita zilizoko katika halmashauri ya mkoa wa Mtwara, yenye jumla ya shule za sekondari 42 zinazoendeshwa chini ya serikali. Kati ya hizi asilimia 18 tu ya shule hizi ndo zenye maabara ya kujifunza Fizikia, Kemia na Baiolojia, kutokana na maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama. 
Akielezea kwamba hali kuwa ni “mbaya,” Kapenjama aliwaambia waandishi wa habari kwamba kukosekana kwa maabara hizo ni kilema kikubwa kwa wanafunzi wanaoazimia kuja kufanya kazi katika tasnia ya sayansi kama madaktari, maenjenia na kadhalika. Kutokana na maelezo ya DC alama ya wastani ya ufaulu kwa wilaya ya Mtwara katika masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari kwa sasa ni asilimia 35.
“Ni kwa sababu hii tuntoa rai kwa wadau wote kutoka katika sekta binafsi na ya umma kuja kutuunga mkono katika kuchangisha fedha kujenga maabara mapya na kuwapatia vifaa kwa maabara chache ambazo tayari zilishajengwa ili kuweza kuwawezesha watoto wetu kufurahia masomo ya sayansi na wakati huo huo kuweza kutimiza ndoto zao ya kuwa wanasayansi bora duniani,” alisema 
Harambee hiyo inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala, itafanyika Ijumaa hii na itajumuisha kampuni na watu binafsi, pia kutakuwa kuna mnada wa bidhaa na vitu mbali mbali kama michoro ya Kiafrika, Yakimakonde na mnada wa safari za kitalii nchini, yote haya ni kwa ajili yakuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara 43 katika sekondari mbali mbali hapa wilayani, alisema Kapenja

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.