Thursday, December 18, 2014

FUNGA MWAKA--TIZAMA VIDEO WABUNGE WA KENYA WALIVYOTWANGANA LEO BUNGENI

Wabunge wa Kenya wamepigana ngumi, kun'gatana na kuoneshana ubabe zaidi bungeni kufuatia kutofautiana juu ya muswada tatanishi wa usalama 

Wabunge wa upinzanzi walipinga muswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni na kukatiza shughuli Bungeni humo

Mapendekezo ya muswada unaopingwa ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali huku uchunguzi ukiendelea.

Wabunge wa upinzani wanapinga muswada huo wenye utata kuhusu usalama maana wanasema unakiuka uhuru wa wakenya

Muswada huu umekuja baada ya kutokea mashambulizi yaliyofanywa na Al Shabaab wakitaka wanajeshi wa Kenya kuondoka Somalia

No comments: