Monday, December 29, 2014

JUKATA--RAIS KAMA UNAMPENDA MUHONGO MPE KAZI SHAMBANI KWAKO SIO UWAZIRI

Makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania JUKATA ndugu HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu mambo mablimbali yaliyojiri mwaka 2014
 Jukwa la katiba nchini Tanzania JUKATA limemtaka  rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwachkulia hatua mara moja wahusika wote waliotajwa kuchota pesa za account ya TEGETA ESCROW ikiwa ni pamoja na waziri wa nshati na madini nchini Tanzania Sospeter Muhongo.

        Hayo yamesemwa leo jijni Dar es salaam na makamu mwenyekiti wa jukwaa hilo ndugu HEBRON MWAKAGENDA wakati akizungumza na wanahabari juu ya matukio mbali mbali ya kikatiba yaliyojitokeza nchni Tanzania kwa mwaka 2014 tukiwa tunaelekea kuuanza mwaka mpya wa 2015.
Amesema kuwa vitendo vya wizi wa mabilioni na ufisadi mkubwa nchini ni doa kubwa kwa sura ya nchi ambapo rais anapaswa kuchukua hatua mara moja bila kujali chama wala itikadi,wala urafiki na mtu yoyote.
        
          “lazima rais awe mkali kama anampenda sana waziri muhongo na anapenda kumpa kazi basi akampe kazi ya kulima kwenye mashamba yake huko ila sio hii ya kuwaongoza watanzania kwani imeonekana wazi kuwa ameshindwa kulitumikia taifa”.amesema makagenda

        Aidha akzungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni nchini Tanzania amesema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na vitendo vya ukiukwaji wa sheria ambapo vilishughudiwa katika maeneo mengi, na maeneo mengine watu wakitoroka na masanduku ya kura jambo ambalo amesema kuwa sio ishara nzuri kwa nchi ya kidemocrasia kama hii.

         Aidha amesema kuwa vitendo hivi vyote ikiwa ni pamoja na  fujo sizizo na msingi katika chaguzi,pamoja na ufisadi wa escrow vyote hivi ni kuporomoka kwa maadili kwa watanzania ambapo amesema kuwa rasimu iliyokataliwa na bunge ilikuwa inapendekeza vifungu vya maadili lakini vifungu hivyo vyote vimenyofolewa katika katiba pendekezwa.
Katika hatua nyingne akizunguzia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya amesema kuwa sasa jukwaa la katiba Tanzania linapendekeza kuwa hatua zote zilizobaki za mchakato huu ziahirishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,ambapo itakuwa ni jukumu la rais mpya ajaye kuanza upya mchakato huo,ambapo amesema kuwa sababu kubwa za kuahirisha mchakato huo ni kutokana na ukweli kwamba Tanzania sasa inakabiliwa na  michakato muhimu kama uandikishwaji wa vitambulisho vya taifa,sakata la escrow,pamoja na uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR.



No comments: