Monday, December 22, 2014

KAULI YA ZITTO NA KAFULILA NA WENGINE BAADA YA HOTUBA YA RAIS JANA



From David Kafulila, Mb

 1.Hoja kwamba pesa zilitolewa kwa uamuzi wa hukumu ya sept5.2013 sio sahh kwasababu hukumu ilisema ALL AFFAIRS OF IPTL SHOULD BE HANDED TO PAP. 


Haikusema kama escrow monies ni party of affairs of IPTL kwasababu zilikuwa kwenye mgororo. hoja ya kusema hukumu ilisema ilikuja baada ya kikao cha Oct8.2013 kunduchi beach hotel ambacho kiliongeza maneno kwenye hukumu kwa kusema ALL AFFAIRS OF IPTL INCLUDING RECEIBLES FROM ESCROW AC SHOULD BE HANDED TO PAP. Huko ni kupotosha hukumu kwani hela za escrow zilikuwa na mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na PAP kununua IPTL haimanishi mgogoro kati ya IPTL na Tanesco umekwisha bali PAP ingechukua nafasi ya IPTL kwenye mgogoro wa pesa za escrow. hili Rais kapotoshwa. 

2. Kusema Muhongo atamtoa bada ya uchunguzi wake ikulu kukamilika ni mbinu ya kumlinda kwani mbona mawaziri wanne waliohusika ktk oparesheni tokomeza ripoti ya bunge ilitosha rais kutengua uteuzi wao na kisha rais akaunda tume ya rais uchunguzi. kwann kwa Muhongo inakuwa kinyume chake? 


3. Bunge liliazimia mamlaka ya uteuzi ichukue hatua dhidi ya Maswi. Rais anasema suala la Maswi ameliacha kwa mamlaka ya nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Hapa Rais amekwepa Jukumu lake kwani yy ndio anateua na kufukuza Makatibu wakuu. pia suala hili sio jipya kwa Katibu Mkuu Kiongozi ingetosha awe amekwisha kuchukua hatua za kinidhamu siku nyingi kama TRA walivofanya kwa wahusika tawi la Ilala.

 4. Hoja kwamba kutaifisha mitambo ya IPTL kutakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu kwa mujibu wa ripoti ya CAG, PAP alifanya utapeli wa kughushi katika umiliki wa IPTL hivyo sio mwekezaji mwadilifu hivyo kutaifisha haiwezi kutisha wawekezaji. pia ifahamike kwamba wawekezaji wengi wanatoka Ulaya na Amerika na nchi hizo ndio zimezuia misaada kutaka serikali itekeleze mazimio ya Bunge na mazimio ya Bunge ni pamoja na kutaifisha mitambo hiyo. sasa inawezekanaje nchi hizo zinazotaka serikali itekeleze mazimio kwamba ndio zikimbie kuwekeza kwa sisi kutekeleza mazimio husika? hapa ni namna ya kulinda matapeli wanaokuja kwa jina la wawekezaji 

5.Hoja kwamba mikataba ikiwa wazi itakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu tatu; a. Nchi nyingi sasa duniani mikataba ipo wazi na mfano rahisi ni Ghana na bado wawekezaji hawajakimbikia kwasababu hiyo. Ndio utekelezaji halisi wa itifaki ya OPEN GOVERNANCE ambayo Tanzania tulisaini b. Kipengele cha Usiri(Confidentiality clause) kwa mikataba yote kinasema mkataba utakuwa siri isipokuwa kwa pande za mkataba(parties of contract) na kwa mahitaji ya dola( statutory purpose). sasa statutory purpose maana yake ni mahitaji ya Serikali, Bunge na Mahakama. sasa tatizo la sasa ni pale serikali inapokataa kutoa mikataba kwa bunge kwa hoja ya kipenge cha usiri(confidentiality clause) wakati kipengele hicho kinaruhusu Bunge kuwa na mamlaka ya kuona mikataba kama part of state organ c. Pia wawekezaji hawa wanaposaini mikataba hapa wanakwenda kutafuta mitaji kwenye masoko ya mitaji kwao(stock markets). Kule kwenye masoko ya mitaji wanaweka wanalazimika kuweka mikataba hiyo wazi na wanaweka. hivyo kwa dunia ya leo ni aibu kuendelea kufanya mikataba kuwa siri.

 6. Hoja ya kodi. TRA walidai kodi kwa barua kwenda BOT. na Werema ndio aliandika barua kukataa kodi. Kwakuwa CAG alikiri ktk ripoti kuwa kodi ilipaswa kulipwa kiasi cha 23bn mana yake alosema kodi isilipwe anapaswa kuchukuliwa hatua za kutaka kusababisha hasara hiyo. ikumbukwe Basil Mramba yupo mahakamani mpaka sasa kwa kesi ya kusababisha hasara ya 11bb. inawezekanaje hawa waishie kujiuzulu? 

7. Mwisho kauli ya Mhe Rais kuwa fedha zile ni za IPTL kwasababu tu ziliwekwa kwenye escrow na Tanesco badala ya kulipwa moja kwa moja kwa IPTL kutokana na mgogoro sio sahh kwasababu pesa ya mgogoro kati ya Tanesco na IPTL haiwezi kuwa ya IPTL mpaka mgogoro umalizike na mwenyewe amekiri kuwa mpaka pesa hizo zinatolewa mgogoro ulikuwa haujamalizika. ni kwa mantiki hiyo pesa hiyo haikuwa sahh kuita ya IPTL. pia hapa niongeze kwamba Mgogoro wa IPTL kutoza zaidi Tanesco capacity charge unamanisha ni dhuluma ya IPTL tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 kama Mhe Rais alivosema. Hii ni kwasababu mgogoro wa IPTL ku overcharge Tanesco kwenye capacity charge msingi wake ni udanganyifu wa IPTL ktk mtaji na hivyo hesabu yake inapaswa kuzingatia tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 escrow ilipofunguliwa. Hii inakaziwa na Uamuzi wa mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ( International Centre For Setllement Of Investment Disputes-ISCID) wa Feb12. 2014. David Kafulila(MB



KAULI  YA  ZITTO  KABWE  KUHUSIANA  NA  HOTUBA  YA  KIKWETE

· Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya Zitto Kabwe, PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM. Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea mtu yeyote. Suala hili sasa naliacha kwa wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe.





KAUL ZA WANASIASA WENGINE KAMA JULIUS MTATIRO NA LEMA ZIKO HAPA

38 mins ·
Rais Amepoteza political legitimacy, amebaki na legal legitimacy
Amepoteza political legitimacy. ..amebaki na legal legitimacy. kapoteza nguvu ya uongozi kabaki na nguvu ya dola ambayo ipo kisheria
Ndio, naweza kusimama na kusema hivyo kwamjibu wa taaluma ya sayansi ya siasa na uongozi.
Amiri Jeshi Mkuu anapingana waziwazi na TRA,TAKUKURU, CAG, BUNGE, na PAC? Anasema pesa za escrow hakuna za umma??
Hii inatafsiriwa kuwa kiongozi mkubwa kabisa katika taifa Amesha amua udikteta hadharani, Amiri Jeshi mkuu keshasema mbele ya waitwao wazee wa Dar, Hakuna mwenye cheo juu yake wakutengua kauli hiyo zaidi ya kusubiri vitendo vya kijeshi.
Katika myumbo wa itifaki ya kirais (PPC), ikulu ya Dar es Salaam ipo katika Def Cond 03 kwa sasa kufuatia kauli za ghiriba, dhihaka na vitisho vinavyoliingiza jeshi la nchi katika kinywa cha rais wa nchi kama ulinzi stahiki wa mamlaka yake.
Hapa kwa wale msiojua nitafafanua kidogo kwa faida ya wengi.
Def Cond ni kipimo kinachotumika kupima hali ya hatari katika nchi, mamlaka za utawala nk,
Katika PPC Def Cond maranyingi hupimwa kutokana na kauli za mtawala (vitisho) dhidi ya anaowatawala, linapotajwa jeshi mara ya kwanza huwa ni Def Cond 01, mara ya pili huwa Def Cond 02, mara ya tatu ni Def Cond 03, na nne na tano huwa ni vita rasmi.
Sasa mara yakwanza Jakaya kalihusisha jeshi na hofu ya umma pale bungeni Dodoma, mara ya pili Lukuvi pale Dodoma kanisani, ya tatu Jakaya pale PTA, Kiasha rais huyu huyu akasema hawajui wamiliki wa Dowans, ajabu siku Dowans inauzwa kwa Syimbion Kikwete huyuhuyu ndie akawa shahidi na leo anasema pesa ya escrow hauna chenji ya umma. Nini kitafuata?
Kuna njia mbili tu zinazoweza kutumika kwa sasa, nazo ni:

Ama kuishawishi system ikubali mabadiliko au kuendesha vuguvugu ambalo bahati mbaya linaweza kugharimu maisha ya watu kama system ina resist. Kuna wazee wengi wenye heshima na hekima kubwa wamechoka kabisa utawala huu ingawa hawawezi kuhama
Muungano ndio asili yetu, mioyoni mwetu. Waliosema tukikubali vyama vingi mwaka 1992 nchi itaingia vitani sasa wamekuja na wimbo mpya wa tukikubali serikali tatu Jeshi litapindua nchi. Wakati ule hawakujipa usumbufu kueleza namna gani tunaweza kuingia vyama vingi bila kuleta vita kama ambavyo leo hawajipi usumbufu kueleza namna tunavyoweza kwenda serikali tatu bila kuvunja Muungano au Jeshi kuchukua nchi. Tutaongoza watu kwa hofu mpaka lini? Ni aibu chama cha siasa na mwenyekiti wake ambae ni rais wa nchi kujigeuza kampuni ya ku supply hofuuu...
FABIAN SOCIETY ilianzishwa na wenye fedha kuhakikisha transformation badala ya revolution duniani..ndio waliombeba sana Mwalimu Julius Nyerere kumjenga alivokua. Ms Weaken alikuwa sehemu ya familia hiyo, ipo nyaraka ya urithi wake alomwandikia Julius Nyerere
Hapa tulipo inapaswa business community & religious community waone hali ya sasa ambayo Jakaya na ccm yake wamepoteza kabisa political legitimacy kiasi watu hawataki kulipa hata kodi halali wasaidie transformation kuepusha revolution
Tumuombee Jakaya Kikwete aepuke na wema na aendelee na wabaya wake wanaomshauri mabaya kwa faida yao hata taifa likianguka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wao hawajali.
Miaka hamsini na tatu ya Muungano wa wa uongo wa ikulu, vitisho, mauaji, uongo na ulaghai imefika mwisho.
Tanganyika Huru na Zanzibar Huru ni msingi wa Muungano imara wa Shirikisho la serikali TatU





TATHMINI YANGU, HOTUBA YA RAIS KIKWETE - WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ESCROW.
1. Nilitarajia angezungukazunguka ili kujaribu kuokoa mwizi huyu au yule - Imekuwa hivyo.
2. Kwa kiasi kikubwa maazimio ya bunge ameyakwepa kwepa tu, ilimradi asiyatekeleze kabisa au akitekeleza iwe hivyo nje ya wakati.
3. Rais ameshindwa kuongea kama mkuu wa nchi, kuwaonesha watendaji na washirika waje kuwa anachukia rushwa, haitaki na anaipiga vita. Kila aliyehusika na wizi wa fedha hizi au mgao wake, rais hasemi kwa uwazi kuwa amevunja taratibu za uongozi, anazungukazunguka.
4. Bodi ya TANESCO ilipaswa kufukuzwa kazi, si kuacha ati imalizie muda wake kwa sababu uko ukingoni. Mchezo huu ni kama ule wa EPA, badala ya kuwaadhibu wezi na kuwaondoa madarakani , wanaombwa warudishe fedha tu.
5. Rais anaonekana hajui msingi wa uchunguzi wa ripoti ya CAG na majumuisho ya PAC. Au amepotosha kila kitu kimakusudi, anahitaji uchunguzi mpya kuchunguza nini ambacho vyombo vya serikali na bunge havijachunguza?
6. Inaonesha wazi kuwa, rais hayuko tayari kuona washirika wake walioiba fedha au kunufaika nazo, wakifikishwa mahakamani.
7. Amejaribu kuonesha ati kashfa hii walioshughulikia ni CCM, na kwamba kama wangeamua kuiacha isingefika hapa ilipo. Rais anasahau kuwa kashfa hii iliibuliwa na gazeti ka THE CITZEN na mbunge DAVID KAFULILA (NCCR) na kusimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, na kwamba wabunge wa CCM walikuwa mbogo baada ya kuona watanzania wamekasirika.
8. Inaonesha kuna mgawanyiko mkubwa sana serikalini, na mambo mengi ambayo Rais kayasema leo yalikywa hayajaamuliwa vizuri, ni kama washauri wake walimuachia yeye mwenyewe amalizie, maana waliona watajikaanga kujaribu kukwepa maazimio ya bunge ambayo yako wazi na yalifikiwa baada ya uchunguzi mkubwa.
9. Kikwete ataondoka madarakani huku 9|10 ya maazimio ya bunge hayajatekelezwa.
10. Viongozi wa CCM, Kinana na wenzake, watakuwa hawajaridhishwa kabisa na maamuzi ya JK, ukizingatia kwamba wamekuwa wakizunguka nchi kusisitiza kuwa watu wote walionufaika na fedha za ESCROW washitakiwe na wanyang'anywe mali zao. Pia rejea kauli za NKM wa CCM, Mwigulu Nchemba, wakati akiwa bungeni.

J. Mtatiro,

Jtatu, 22 Dec 2014,

Dar Es Salaam






"Ukiwa unasema ukweli huhitaji muda

mrefu kutoa maelezo"

News Feed

Our Leaders Must move away from culture of denials, cover-ups and proxies and deal honesty, sincerely and transparently with Tanzanians to regain their trust and confidence.

Tanzanians are no fools, they can see, they can hear, they can talk among themselves, they can think and they can act in the interest of their country.
[ largely borrowed from General Obasanjo's letter to President Jonathan of Nigeria ]. Found the words very relevant at the current circumstances in Tanzania



Hii ilikuwa nafasi ya mwisho ya JK kurudisha Political Legitimacy yake kwa watanzania baada ya kuipoteza kwa muda mrefu.. Bahati mbaya ameshindwa kuirudisha na wala hajutii. Poor him.!


No comments: