Saturday, December 6, 2014

CHUO KIKUU HURIA CHAFANYA KWELI KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI-SOMA HAPA KUJUA

Kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi  Chuo Kikuu Huria upande wa Kinondoni Mussa h Omari kushoto ni Rais Mwezake  wa Chuo hicho upande wa Temeke Mganwa Nzota wakitoa Elimu kuhusu Maambukizo Mapya ya Ukimwi Leo Jijini Dar Es Salaam
Wanafunzi wa Chuo chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kampus ya temeke wakisikiliza Jambo kwenye Semina hiyo
Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Kampus ya Temeke David Malangalila akiwaelekeza Jambo viongozi wenzake katika Semina hiyo
Viongozi wa juu wa Serikali ya Wanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Huria wakimasikiliza Mtoa Mada Mussa h Omari

Na Karoli Vinsent       
Wito umetolewa kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu huria nchni kuuchukulia Ugonjwa wa Ukimwi kama Janga ambalo linahaja ya kupigwa vita kwani ugonjwa huo umetajwa kuwa ni kikwazo katika kufikia malengo ya wanafunzi katika chuo hicho kikuu.

     Rai hiyo imetolewa  mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu huria nchini kampus ya Temeke Dk Jakrini Bundala wakati Akifungua Semina  kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusu maambukizi Mapya ya Ukimwi,ambapo Dk Bundala alisema licha ya chuo hicho kuzarisha wasomi mbalimbali nchini na nje nchi pia  wanawajibu wa kuijenga jamii isiyokuwa na Maambukizo mpya ya Ukimwi ndio maana chuo hicho  wameandaa semina hiyo kwa wanafunzi kila mwaka.

       Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu huria Kampus ya Temeke Mganwa Nzota aliushukuru uwongozi wa Chuo Kikuu huria kwa kuandaa Semina ya kupiga Vita Maambukizi Mapya ya ukimwi kwani kufanya hivyo itasaidia kuijenga Jamii ya wanafunzi hao kutokuwa na Maambukizi ya Ukimwi.

No comments: