Wednesday, December 17, 2014

LHRC--WAZIRI GHASIA WAJIBIKA,UCHAGUZI ULIKUA NA KASORO NYINGI

Afisa uangalizi wa uchaguzi kutoka LHRC HAMIS MKINDI akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu kazi hiyo waliyoifanya na kasorozilizojitokeza katika uchaguzi huo
Baada ya kufanya uangalizi kwa njia za kisasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jumapili nchini Tanzania kituo cha sheria na haki za binadamu nchni LHRC kimeibuka na kudai kuwa uchaguzi huo ulijawa na kasoro nyingi ambazo zinafanya uchaguzi huo upoteze uhalali kwa kuwa ulikiuka misingi ya katiba na haki ya wananchi ya kupiga kura.
Wakili HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi huo ambapo amesema kuwa ni jambo la aibu uchaguzi unakumbwa na kasoro nyingi kama kukosekana kwa karatasi,au majina kuandikwa kwa kalamu pia kuchapishwa jambo ambalo amesema kuwa ni aibu kwa taifa kama tanzania
Akizungumza na wanahabari leo afisa muangalizi wa uchaguzi kutoka LHRC wakili HAMIS MKINDI amesema kuwa kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi huo zimeathiri kwa kiasi kikubwa zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wameitaka serikali kupitia wizara husika ambayo ni ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM kuwajibika kwa kushindwa kusimamia uchaguzi huo kikamilifu.


Akizitaja kasori hizo amesema kuwa kushindwa kwa wananchi kupiga kura,kukosekana kwa karatasi za kupigia kura,kufungwa kwa vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi bila sababu ya msingi,kukosewa kwa karatasi za kupigiwa kura kukosekana kwa karatasi za kupigia kura,na pia kukusekana kwa majina ya wapiga kura ni kasoro ambazo zinaonyesha wazi kuwa zoezi hili lilifanyika bila maandalizi na kwa lugha nyingine ni kukurupuka.

Aidha LHRC wamelaani vikali vitendo vya vurugu zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu na serikali ambapo taarifa za waangalizi wa kituo hicho zinaonyesha kuwa vurugu nyingi zilitokana na udhaifu wa usimamizi na wanachi kuamua kufanya vurugu baada ya kuona mambo hayaendi kama yalivyotakiwa kwenda.
wabahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini
Pamoja na hayo kituo kimewapongea wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba katika kupiga kura ambapo wamesemakuwa mwaka huu muamko ni mkubwa hasa kwa vijana hali ambayo inatia matumaini kuwa sasa watanzania wameanza kutambua haki yao ya kupiga kura


No comments: