Tuesday, December 16, 2014

UCHAGUZI WA MITAA--LIPUMBA AIBUKA,AMTAKA RAIS KUTUA MIZIGO YOTE,SOMA ALICHOKIZUNGUMZA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIMU  LIPUMBA  akizungumza na wanahabari mapema leo makao makuu ya chama hicho Buguruni Jijini Dar es salaam

            Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIM LIPUMBA amemtaka Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Rais JAKAYA KIKWETE kuwawajibisha waziri mkuu wa Tanzania mh MIZENGO PINDA pamoja na waziri wa tamisemi mh HAWA GHASIA kwa kushindwa kusimamia vizuri uchaguzi wa serikali za mitaa huku akiwaita kuwa ni mizigo kwa rais na haibebeki.
           
Akizungumza na wanahabari makao makuu ya chama hicho asubuhi ya leo LIPUMBA amesema kuwa chama chake kimesikitishwa sana na mwenendo mzima wa uchaguzi huu pamoja na zoezi nzima la upigaji kura ambapo amesema kuwa zoezi hilo liligubikwa na sintofahamu kadha wa kadha na kusababisha vurugu katika baadhi ya vituo.
      
Akitaja baadhi ya mbinu chafu ambazo amesema kuwa zilifanywa na serikali ili kuwadhoofisha wapinzani ni pamoja na wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa siku moja kabla ua uchaguzi na wengine siku ya uchaguzi,uchaguzi kutokuanza kwa wakati katika maeneo mengi ya Tanzania,uchaguzi kusogezwa mbele bila sababu ya msingi katika wilaya nyingi,pamoja na matukio mengine mengi yakiwemo ya vurugu na uchakachuaji ambapo amesema kuwa ni ishara tosha kua uchaguzi huu haukuwa wa haki.
    
   “ndugu wanahabari lazima mh Rais atumie busara kama anataka kumaliza kipindi chake bila mizigo ni lazima akubali kuitua mizigo ambayo inaonekana wazi kuwa inamuelemea na wa kwanza ni waziri mkuu mizengo pinda ni mzigo ambao lazima Rais akubali kuutua ili mambo yakae sawa”amesema lipumba.
Wanahabari wakisikiza kwa makini
             Amesema kuwa matukio yaliyojitokeza katika uchaguzi wa seikali za mitaa mwaka huu yamedhihirisha wazi tamko lao ambalo wamewahi kulitoa kuwa serikali wamekurupuka kutangaza uchaguzi wa serikali za mitaa na hawajajipanga kusimamia uchaguzi huo.
             
Aidha amesema kuwa wananchi sasa wamechoka na ufisadi wa mali za umma  unaondelea na wameamua kufanya mabadiliko hivyo hivyo huku akiwataka wanachi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kufanya mabadiliko hayo.
        
Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania ulifanyika jumapili ya wiki ya jana ambapo iliripotiwa kuwa na dosari nyingi katika maeneo mengi jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi kuwa wizara husika imeshindwa kusimamia uchaguzi huo


No comments: