Wednesday, January 14, 2015

ESCROW--- KAZI IMEANZA,WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO



Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TanzaniaTAKUKURU imewaburuza mahakamani  baadhi ya watuhumiwa wawili wanao kabiliwa na Kashfa ya uchotwaji Fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow Kisutu Kisutu Jijini Dae es Salaam


Waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ni Mhandisi TEOFILI JOHN kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambaye anakabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya shilingi milioni 161.

Alipokea fedha hizo sehemu ya akaunti ya Tegeta Escrow kutoka kwa JAMES RUGEMARILA yeye akiwa msimamizi wa mradi wa mpango wa umeme vijijini.

Mtuhumiwa wa pili ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi Bwana RUGWENZIBA TEOFILI aliyepokea shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusimamia kesi za IPTL.

Endelea kutufuatilia tutakujuza kila Hatua.

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA TAMBARARE HALIS BLOG

No comments: