Sunday, January 25, 2015

ESCROW YAWAIBUA WAISLAM NAO LEO,SOMA HII

SHEKH RAJAB KATIMBA ambaye ni katibu wa shura ya maimamu nchini Tanzania akizngumza na wanahabari mapema leo nje ya mkutano huo
Baada ya aliyekuwa waziri wa nishati na madini nchini Tanzania profesa SOSPETER MUHONGO jana kutangaa rasmi kuachia ngazi kutokana na tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni kwenye account ya ESCROW wadau mbalimbali wametoa maoni yao juu ya sakata hilo na jinsi linavyoshughulikiwa.

Mmoja kati ya watu waliozungumza na mtandao huu ni SHEKH RAJAB KATIMBA ambaye ni katibu wa shura ya maimamu nchini Tanzania ambapo leo wanafanya kongamano la maimamu jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwakumbusha waislamu wote nchini juu ya majukumu yao katika jamii kwa ujumla.

Akizungumza nje ya kongamano hilo shekh RAJAB amesema kuwa kitendo cha mawaziri na viongozi waliohusika na ESCROW kutangaza kujiuzulu kimya kimya bila hatua zaidi kufwatwa ni usanii mkubwa kwan sio utatuzi wa sakata hilo na badala yake wanapumzika baada ya kufanya ufisadi huo.

Amesema kuwa njia sahihi ni kuwashuhulikia wahusika kwa mujibu wa sheria na sio kujiuzulu pekee kwani haitoshi.
“nitolee mfano swala la jana la waziri MUHONGO kujiuzulu na kusisitiza kuwa yupo safi kabisa,na wakati yeye hana mamlaka ya kujisafisha ila kuna vyombo ambavyo vinaweza kusema kuwa yuko safi ni kitendo cha kuwahadaa watanzania”amesema shekh katimba.


Maimam mbalimbali ambao wamehusdhuria katika semina hiyo
Ameongeza kuwa hatua zinazoeendelea kuchukuliwa na serikali pamoja na mamlaka husika juu ya sakata hilo ni za kupongezwa japo kuwa zimechelewa sana na watu wameiba na kujulikana zamani ila wamekuwa wakiachwa kimya kimya
Katika hatua nyingine shekh KATIMBA ameendelea kusisitiza kuwa mchakato wa kupakana kwa katiba umejawa na usanii na utapeli mkubwa ambao uko wazi huku akitolea mfano swala lao wanalolidai kwa muda mrefu la kupatikana kwa makahakama ya kadhi ambalo limekuwa likipigwa kalenda kila linapoibuka ambapo amesema kuwa wataendelea kudai hadi kieleweke.
Amesema kuwa kutokana na wao kutokusikilizwa juu ya madai yao kwenye katiba sasa wanajipanga kuwahamasisha watanzania na waislam wote kwa ujumla kuususia mchakato wa katiba mpya kwani hauna manufaa kwa watanzania wote bali ni kwa watu wachache tu.

No comments: